Tuesday, August 19, 2014

CHUO KIKUU CHA BAGAMOYO CHAWAFUNDA MAOFISA BIASHARA WA NCHI 15



CHUO KIKUU CHA BAGAMOYO CHAWAFUNDA MAOFISA BIASHARA WA NCHI 15
Mtaalamu wa kujadili mikataba kutoka World Trade Organization (WTO), Prof. Dickson Yeboah akitoa mada jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa Kimataifa wa kuwajengea uwezo maofisa wa serikali kutoka nchi 15 za Afrika Mashariki, Afrika ya Kati na Afrika Kusini kuhusu uandikaji wa mikataba inayohusu Uwekezaji na Biashara. Mkutano huo umeandaliwa na Chuo Kikuu cha Bagamoyo.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo.

Na Happiness Katabazi

CHUO Kikuu cha Bagamoyo (UB), kimesema kitaendelea kuandaa mafunzo  ya jinsi ya Kutengeneza mikataba na wawekezaji  kwa maofisa wa serikali za nchi zinazoendelea ili serikali hizo ziondokane na tatizo la kuandika mikataba ya uwekezaji ambayo haiziletei faida nchi zao.

Akizungumza na Katika  Mafunzo yanayoshirikisha wataaluma wa masuala ya Biashara toka nchi 15 yanayofanyika Katika Hotel ya Habour View Dar Es Salaam ambapo Mafunzo hayo yameandaliwa na Chuo Kikuu Cha Bagamoyo na kufadhiliwa na Chuo Kikuu Cha Nordic Africa Institute of the University of Uppsala Cha nchini Sweden, Mkuu wa Shule ya Biashara na Utawala (UB), Dk.Lenny Kasoga Alisema Mafunzo ya wiki mbili yameusisha  maofisa wa juu wa serikali mbalimbali ambao ni wataalamu wa fani ya Biashara toka nchi 15.

Dk.Kasoga alisema Leo Dunia ipo Karne  ya 21 lakini bado nchi  zinazoendelea ambazo  zimegundulika Kuwa na utajiri  mkubwa  zimejikuta zikiingia mikataba mibovu na wawekezaji KWA Sababu tu nchi hizo Hazina wataaluma serikalini ambao wamebobea Katika kufanya mijadala ya Kibiashara na wawekezaji na jinsi ya kuandika mikataba hiyo.

"Kwa kukuona tatizo Hilo sisi UB, tumeandaa Mafunzo haya ambayo yamewapa mwanga maofisa Hao waandamizi toka serikali za nchi 15 ambapo Mafunzo tuliyowapatia watayapeleka Katika serikali zao na vyuo vyao ili waweza kuandaa mitaala Katika vyuo vikuu vyao NGazi ya Shahada ya Pili ili watu wasome' Alisema Dk.Kasoga.

ALizitaja nchi zinazoshiriki Mafunzo ambayo ni ya kwanza kufanyika nchini  ambayo yanatarajiwa Kufungwa Ijumaa ya wiki hii na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk.Shukuru Kawambwa  Ni Mwenyeji Tanzania na Zanzibar, Madagascar,Mozambique, Rwanda,Malawi,Zambia, Burundi, Uganda, Ethiopia ,Kenya, Kongo, Malawi na Lesotho.

Kwa upande wake Profesa Francis Matambalya toka Chuo Kikuu Cha NAI, Uppsalla nchini Sweed, alisema chuo chao wameamua kufadhili UB iendeshe Mafunzo hayo kwasababu wanaamini UB ninauwezo wa kuendesha Mafunzo na kwamba Tanzania pia ambayo Katika Mafunzo hayo wamewasilisha na maofisa Biashara toka Wizara ya Viwanda na Biashara nayo inamkabili na Changamoto hiyo.