Wednesday, October 15, 2014

Bayport Tanzania yaleta kicheko kwa watumishi wa umma



Bayport Tanzania yaleta kicheko kwa watumishi wa umma
 Meneja Biashara wa Bayport Tanzania, Thabit Mndeme kushoto; na Meneja Masoko na Mawasiliano (katikati), Ngula Cheyo waki zinduwa Mkopo wa Bidhaa, Bayport Head office Daressalaam.
=====  =====  =====
TAASISI ya kifedha ya Bayport Tanzania, leo imezindua huduma mpya ijulikanayo kama Mikopo ya Bidhaa ikiwa na lengo la kurahisha utendaji kazi wa watumishi wa umma na wafanyakazi wote wa kampuni zilizoidhinishwa na Bayport.

Uzinduzi huo uliofanyika jana, umeonyesha matumaini mapya ya Watanzania wanaosumbukia usafiri katika vituo vyao vya kazi, hususan maeneo ya mikoani ambako mara kadhaa kumesikika malalamiko ya maisha magumu ya watumishi wa umma.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Meneja Biashara wa Bayport Tanzania, Thabit Mndeme, alisema kwamba  ni wakati wa kukuza uchumi wan chi kwa kuhakikisha kuwa watu wote wanafanya kazi kwa bidii na shauku yote.

Alisema wapo watumishi ambao wanaishi kwa tabu kutokana na changamoto ya usafiri na mahitaji mengine ya kijamii, hivyo kwa kupatikana hudumaa mpya ya kukopeshwa pikipiki bodaboda ni jambo zuri kwao.

''Bayport tumekaa na kuangalia namna gani Watanzania wataendelea kufanya kazi kwa moyo na kukuza uchumi wetu, tukaona sambamba na kuwakopesha fedha kama tunavyofanya, pia tuwakopeshe bidhaa kama vile Boxer, Toyo na Lifan.

''Zote hizi zitakuwa kwenye mpangilio mzuri sambamba na kuzikatia huduma ya bima, kuzifanyia servise mara tatu bure, garantii ya mwaka mmoja, huku mkopaji akitakiwa kulipa kwa miezi 36 sawa na miaka mitatu,''alisema Mndeme.

Naye Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Tanzania, Ngula Cheyo, alisema kuwa mikopo hiyo mipya itapatikana kwa masaa 24, huku ikipatikana pia kwa mikoa yote na wilaya zote kwenye ofisi za Bayport Tanzania.

''Tunawaomba watu waendelee kuiunga mkono Bayport kwa kuhakikisha kuwa wanachangamkia fursa hii ya mikopo ya bidhaa ambayo tumeianzisha ili kuwafanya watumishi wa umma na wafanyakazi wengine warahisishiwe utendaji wao wa kazi,'' alisema Cheyo.