Tuesday, October 09, 2012

Bodi ya Utalii Nchini Tanzania yamtambulisha mpishi maarufu Duniani kutoka nchini India Sanjeev Kapoor ambaye amekuja nchini kwa ajili ya kuandaa vipindi vya runinga ambavyo vitahusu mapishi ya vyakula vyaasili ili kutangaza utalii wa kiutamaduni.



 Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Nchini Dkt. Aloyce Nzuki (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na mpishi maarufu Duniani kutoka nchini India SanjeevKapoor (wa pili kulia) mara baada ya kumalizika kwa mkutano baina yao na waandishi wa habari uliohusu umuhimu wa vyakula vya asili katika sekta ya utalii uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Meneja Mkuu wa Hoteli ya Serena Daniel Sambai na kushoto ni Mkurungezi wa Performance Ltd. Tanzania Runjiv Kapur.
 Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Nchini Dkt. Aloyce Nzuki (kushoto) akimtambulisha mpishi maarufu Duniani kutoka nchini India SanjeevKapoor kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam ambaye amekuja nchini kwa ajili ya kuandaa vipindi vya runinga ambavyo vitahusu mapishi ya vyakula vyaasili ili kutangaza utalii wa kiutamaduni. Mpishi Kapoor Atakuwepo nchini kwa muda wa wiki mbili kwa ajili ya kuandaa vipindi hivyo.
Baadhi wa wageni waalikwa na mwaandishi wa habariwakimsiliza Mpishi maarufu Duniani kutoka nchini India SanjeevKapoor (hayupo pichani) akielezea umuhimu wa vyakula vya asili katika sekta ya utalii wa nchi Mpishi Kapoor atakuwepo nchini kwa muda wa wiki mbili kwa ajili ya kuandaa vipindi vya runinga ambavyo vitahusu mapishi ya vyakula vyaasili ili kutangaza utalii wa kiutamaduni nchini India. Picha na Anna Nkinda –MAELEZO