Tuesday, October 09, 2012

WAZAZI KATA YA MADIBIRA WAFIKISHWE MBELE YA SHERIA KWA KUSHINDWA KUPELEKA WATOTO WAO SHULE



KAMATI YA  ya maendeleo ya Kata ya Madibira Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya imewafikisha kwenye baraza la kata wazazi 14 ambao wameshindwa kuwapeleka watoto  wao kuanza kidato cha kuanza kwa makusudi ili waweze kuchukuliwa hatua.

Mwandishi  wetu kutoka Mbeya Esthr Macha anaripoti  kuwa ,Hatua hiyo imefuatiwa baada ya kikao cha kamati ya maendeleo ya Mkoa wa Mbeya (RCC) kilichoketi April  5 mwaka huu kuamuru wazazi  wote kukamatwa kwa kosa la kushindwa kuwapeleka shule kwa sababu mbali mbali.

Kauli hiyo imetolewa jana na Kaimu Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali ,Bw.Elia Mhecha wakati alipozungumza na gazeti kuhusiana na wazazi ambao wameshindwa kuwapelaka shule watoto wao licha ya kufaulu.

Alisema kuwa zoezi hilo lilianza mara moja na kugundua kuwa watoto nane  hawakuwa wameanza masomo yao ya kidato cha kuanza licha ya kufaulu vizuri katika shule ya sekondari Madibira.

“Ndugu mwandishi baada ya kusumbuliwa sana wazazi wa wanafunzi hawa ilibidi wawapeleke watoto wao kuanza masomo yao ya kidato cha kwanza lakini bado hatua za kisheria zinaendelea  ili iweze kuwa fundishi kwa wazazi wote ambao wamekuwa wakiwakilisha nyumbani watoto licha ya kufaulu ,hili nadhani litasaidia wazazi wengine hata kama wamewaleta shule lakini sisi msimamo wetu ni kuhakikisha kuwa kila motto anayefaulu anaingia kidato cha kwanza”alisema Bw.. Mhecha.

Aidha alisema kwa wale ambao walikuwa wamefaulu na kwenda shule binafsi serikali ya wilaya haikuwa imewafatilia kwakuwa ilibaini kuwa walikuwa masomoni tayari kwa hawa wengine  imebidi  mkoa uhaqkikiswhe wanakwenda shule hata kama mzazi hakuwa anataka motto aende shule.

Akizungumza na gazeti hili kuhusu  wanafunzi hao  kutokwenda shule Ofisa Mtendaji wa Kata ya Madibira Bw. Mikidadi Mwazembe alikiri wazazi wa wanafunzi 14 kukamatwa na baraza la kata .

“Sisi baada ya kupata taarifa kutoka kwa Mkurugenzi mtendaji wa wilaya, mimi kama Mtendaji wa kata nilianza mchakato  kwa kuwaagiza watendaji wote wa vijiji kupata orodha ya wanafunzi ambao hawajaanza kidato cha kwanza mwaka huu  na kubaini watoto nane na wazazi wa wanafunzi kuandikiwa barua na kuitwa kwenye baraza la kata “alisema.

 Hata hivyo Bw.Mwazembe alisema kuwa baada ya kuitwa kwenye baraza la kata wazazi hao walikiri kutowapeleka shule watoto wao na baraza hilo kuamuru wazazi kufikishwa mahakamani  mara moja.

Mwisho.