Wataalam wa uchimbaji wa visima virefu vya maji,wakiendela na shughuli hiyo katika eneo la Shule ya Msingi Kwamsanja iliopo katika kijiji cha Kwamsanja ndani ya Jimbo la Chalinze, Bagamoyo mkoani Pwani.Hatua hiyo imekuwa kutokana na ahadi ya iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mh. Ridhiwani Kikwete wakati wa Kampeni za Kuwania Ubunge katika Jimbo hilo.
Shughuli ya upatikanaji wa Maji sasa imekamilika na kinachofuata ni ujengaji wa Tanki kubwa la kuhifadhi maji hayo,ambayo yatatatua kabisa tatizo la maji kwa wakazi wa maeneo mbalimbali ndani ya Jimbo hilo la Chalinze.