Thursday, August 14, 2014

SERIKALI YATAKIWA KUTIMIZA AHADI ZA UJENZI WA ZAHANATI KWA KILA KATA



DSC_0534
Diwani wa kata ya Ololosokwani na Mkurugenzi wa Irkiramat Foundation (RAMAT) Bw. Yannick Ikayo Ndoinyo akiangalia kitanda cha kujifungulia wakimama kwenye Zahanati ya Sero ambayo kwa siku inatibu wagonjwa 50 na zaidi ikiwa na daktari mmoja huku wakazi wanaofuata huduma hiyo kutoka kata hiyo na ya jirani Soitosambu kutembea umbali mrefu kwa Kilometa 7-15 kupata huduma ya afya.(Picha Zainul Mzige)

Na Mwandishi wetu, Ngorongoro

Wakazi wa vijiji vya Ololosokwan, Soit-Sambu, Njoroi na Loipir kata za Ololosokwana na Soit-Sambu wilayani Ngorongoro wanakabiliwa na changamoto kubwa ya huduma ya Afya kwa kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo kwenye kijiji cha Sero huku waathirika wakubwa ni kinamama na watoto.

Umbali wa zahanati hizo imekuwa sababu kubwa ya vifo hususani kwa akina mama wajawazito wanaotaka kwenda kujifungua na watoto halikadhalika wanapozidiwa hufia njiani kutokana na umbali wa zahanati kutoka kijiji kimoja kwenda kingine wanapotakiwa kuwahishwa hospitalini hali inayowafanya kutembea umbali mrefu kilometa 15 hadi kuipata huduma ya zahanati .

Akizungumza na waandishi wa habari Diwani wa kata ya Ololosokwani na Mkurugenzi wa Irkiramat Foundation (RAMAT) Yannick Ikayo Ndoinyo waliotembelea miradi inayofadhiliwa na Shirika la Elimu na Sayansi (UNESCO) wilayani humo alisema serikali haina budi kutimiza ahadi yake ya kujenga Zahanati kwa kila kata nchini Tanzania kuwapunguzia wagonjwa hususan akina mama waja wazito na watoto adha ya kutembea au kusafiri mwendo mrefu kutafuta huduma za afya.

Ndoinyo alisema kuwa tatizo kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma ya afya lipo na kwamba vifo ya wamama na watoto na kutopata huduma zinazotakiwa kwa wakati. Wananchi hupata huduma za afya kutoka Sero ambayo ina umbali mrefu kutoka Ololosokwang au wakati mwingine mgonjwa hupata rufaa rufaa hadi Hospitali ya wilaya ya Waso na iwapo mgonjwa atakuwa katika hali mbaya ni tatizo.
DSC_0532
Gari la wagonjwa lilitolewa na serikali likiwa limeharibika kutoka na miundo mbinu ya barabara na kushindwa kufanyiwa matengezo kwa muda mrefu hali inayomfanya daktari wa Zahanati hiyo kuwafuata majumbani wagonjwa mahututi kwenda kuwapatia huduma za afya.