Mgeni rasmi Mr Leonard Badole Ipuli akishuka kutoka high table kwende kuzindua albamu ya Simama na Mwokozi katika uwanja wa CCM Kirumba leo.
Mc wa shughuli ya leo kutoka Dar es Salaam Mc Tito akimkaribisha Mgeni Rasmi ili aweze kuongea na kuizindua albamu ya Simama na Mwokozi.
Hata Mgeni rasmi akikata utepe kuzindua albamu mpya ya Aic Happy Malampaka leo CCM Kirumba.
Mc Mashikolo akisoma nyimbo zilizomo katika DVD mpya ya Aic Happy Malampaka.
Mc Mashikolo amezishaka na Mzuka baada ya Kutamka kutoa laki Tano kwa ajili ya uzinduzi ya DVD ya Simama na Mwokozi.
Umati wa mashabiki wa muziki wa injili walikuwa katika uwanja wa CCM Kirumba wakiona mambo yanayofanyika uwanjani hapo leo.
Mwonekano wa wapenzi wa muziki wa Gospel.
Kwaya ya Aic Happy Malampaka wakiimba uwanjani leo.
EAGT Msumbiji wakiwajibika stejini.
Aic Vijana Bwiru wakiimba wimbo wenye upako katika uzinduzi wa DVD ya Aic Happy Malampaka.
Upande wa vyombo vya muziki ulikuwa hivi...
Meza ya Wageni rasmi ikiwa imependeza..
Vijana Bwiru.
On Mark, Set Go.....
Aic Happy Malampaka wakishuka ngazi kua stejini kuimba...
Mwonekano wa kina dada wa Malampaka..
Mratibu wa uzinduzi wa Aic Happy Malampaka Mr. Joshua akisoma risala mbele ya Mgeni rasmi leo.
Wadau wa muziki wa Injili wakiangalia matukio mbalimbali uwanjani.
Kwaya ya Aic Happy Malampaka Maarufu kama Wana Geuka wamezindua albamu yao mpya ya DVD iitwayo SIMAMA NA MWOKOZI katika tamasha kubwa la uzinduzi ambao umefanyika katika uwanja wa CCM Kirumba leo.
Akisoma risala ya Kwaya hiyo, Mratibu wa Uzinduzi huo Mr. Joshua amesema hiyo ni mpya yenye ujumbe wa kuokoa mioyo iliyochoka na dhambi na vilebile kuokoa wali dhambini na kusema wao wako tayari kuipeleka injili Tanzania, Afrika, na duniani kote.
Akizindua albam hiyo Mgeni rasmi Mr. Leonard Bapole Ipuli amesem anaipenda kwaya hiyo na kusema kuwa anapenda jinsi wanavyoimba na kusema kuwa yeye pamoja na Wageni wenzake wako tayari kuizindua albamu hiyo.
Mgeni rasmi akiwa ameambatana na wageni wenzake amewatia moyo kwa kuizindua kwa Shilingi Milioni mbili pamoja na wageni wengine kama Mbunge wa jimbo la Sengerema akitoa milioni moja. Jumla ya shilingi milioni tano zimepatikana katika uzinduzi huo ukiachilia uuzaji wa DVD zao mpya.