Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia katika Mkutano wa 20 wa Kimataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, unaoendelea Jijini Lima nchini Peru. Makamu wa Rais alizungumza kwa niaba ya nchi za Afrika kuhusu utekelezaji wa maazimio mbalimbali ya mabadiliko ya tabianchi. Pamoja na mambo mengine Dkt. Bilal alizungumzia namna nchi za Afrika zilivyojizatiti katika maazimio mbalimbali yanayolenga kunusuru majanga yatokanayo na Tabianchi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipiga picha ya kumbukumbu na Mkuu wa Ujumbe wa China, katika mkutano wa Mkutano wa 20 wa Kimataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, Xie Zhenhua, wakati walipokutana kwa mazungumzo baada ya kuhudhuria na kuhutubia katika mkutano huo unaoendelea Jijini Lima nchini Peru, ambapo alizungumza kwa niaba ya nchi za Afrika kuhusu utekelezaji wa maazimio mbalimbali ya mabadiliko ya tabianchi. Pamoja na mambo mengine Dkt. Bilal alizungumzia namna nchi za Afrik zilivyojizatiti katika maazimio mbalimbali yanayolenga kunusuru majanga yatokanayo na Tabianchi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza jambo na baadhi ya viongozi wenzake wakati walipohudhuria katika Mkutano wa 20 wa Kimataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, unaoendelea Jijini Lima nchini Peru, ambapo alizungumza kwa niaba ya nchi za Afrika kuhusu utekelezaji wa maazimio mbalimbali ya mabadiliko ya tabianchi. Pamoja na mambo mengine Dkt. Bilal alizungumzia namna nchi za Afrik zilivyojizatiti katika maazimio mbalimbali yanayolenga kunusuru majanga yatokanayo na Tabianchi.
Picha ya kumbukumbu na wadau wa masuala ya mazingira walipokutana katika viwanja vya kumbi hizo za mikutano. Picha na OMR