Saturday, October 04, 2014

KILIMANJARO PREMIUM LAGER YAKUTANA NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI KUZUNGUMZIA KAMPENI YA “NANI MTANI JEMBE 2”




KILIMANJARO PREMIUM LAGER YAKUTANA NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI KUZUNGUMZIA KAMPENI YA "NANI MTANI JEMBE 2"
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akizungumza na baadhi ya wahariri wa vyombo habari jijini Dar es Salaam mchana wa leo,wakati wa semina ya kuzungumzia uzinduzi wa Kampeni ya Nani Mtani Jembe sehemu ya 2,utakaofanyika kesho tarehe 4 Oktoba 2014 katika viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijini Dar es salaam. 
Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Executive Solutions ambao ndio wanaoratibu Kampeni hiyo ya Nani Mtani Jembe 2,Ibrahim Kyaruzi akizungumza jambo kwenye mkutano huo.
baadhi ya wahariri wa vyombo habari jijini Dar es Salaam wakifatilia kwa makini semina hiyo.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akielezea namna Kampeni hiyo itakavyokuwa ikifanyika.