Kampuni ya Gapco Tanzania Ltd leo hii imezindua kilainishi kipya cha pikipiki kilijulikanacho kama Relstar Alpha 4T Ultra. Uamuzi wa Gapco kuzindua bidhaa hii ni kutokana na ongezeko kubwa la pikipiki nchini haswa kwa matumizi ya kibiashara.
Akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Gapco, Bwana. Macharia Irungu alisema, "Utafiti umetuonyesha kwa sasa watumiaji wamiliki wengi wa pikipiki wanalazimishwa kutembelea gereji mara mbili kwa mwezi kwa ajili ya kurekebisha pikipiki zao. Kupitia kilainishi chetu cha Relstar Alpha 4T Ultra tunawahakikishia wateja wetu kutumia muda mfupi kwenye warsha na kupata maili zaidi kwa pesa zao.
Ongezeko kubwa la pikipiki au bodaboda nchini imeleta pia ongezeko la vilainishi vya pikipiki vyenye viwango vya chini. Kupitia kilainishi kipya cha Gapco wateja wataweza kupata; maili zaidi na akiba wanapoenda kufanya marekebisho kwenye pikipiki zao.
Naye Mgeni Rasmi katika hafla hiyo, Kamander wa Trafiki, Bwana. Mohamed Mpinga aliwaonya watumiaji wa pikipiki kuepukana na vilainishi vya viwango vya chini na pia kuwahimiza kutii sheria za barabarani.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabara Tanzania,Kamanda Mohamed Mpinga na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Gapco Afrika Mashariki, Macharia Irungu wakizindua vilainishi vya GAPCO RELSTARALPHA 4T vya Pikipiki za miguu miwili na mitatu wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa jijini Dar es Salaaam jana.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarania Tanzania,Kamanda Mohamed Mpinga na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Gapco Afrika Mashariki, Macharia Irungu wakipiga makofi mara baada ya kuzindua vilainishi vya GAPCO RELSTARALPHA 4T vya Pikipiki za miguu miwili na mitatu wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa jijini Dar es Salaaam jana.
Picha ya pamja mara baada ya uzinduzi wa vilainishi vya GAPCO RELSTARALPHA 4T vya Pikipiki za miguu miwili na mitatu wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa jijini Dar es Salaaam jana.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabara Tanzania,Kamanda Mohamed Mpinga akimkabidhi William Dafta koti maalum la kuaksi mwanga mara baada ya kuzindua vilainishi vya GAPCO RELSTARALPHA 4T vya Pikipiki za miguu miwili na mitatu wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa jijini Dar es Salaaam jana.
Waendesha pikipiki(maarufu kama Bodaboda) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua vilainishi vya GAPCO RELSTARALPHA 4T vya Pikipiki za miguu miwili na mitatu wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa jijini Dar es Salaaam jana huku wakiwa wamevalia makoti maalumu ya kuaksi mwanga yaliyotolewa na Kampuni hiyo ili kujilinda na usalama wao.