Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nchemba Mkoani Dodoma Bw. Boniface Mandi akifungua Mafunzo ya Vikundi vya Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Nchemba kuhusu Mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.Mafunzo hayo yanatolewa na kuratibiwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nchemba Mkoani Dodoma Bw. Boniface Mandi akiongea na Timu ya Maafisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo kabla ya kufungua Mafunzo ya Vijana wa Wilaya hiyo kuhusu Mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, kulia ni Afisa Vijana Bi Amina Sanga.
Vijana wa Wilaya ya Nchemba Mkoani Dodoma wakimsiliza mwezeshaji (hayupo pichani) Bi. Amina Sanga katika Mafunzo ya Vijana wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kuhusu Mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana
Afisa wa Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nchemba Mkoani Dodoma Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana na kitabu cha Mwongozo Sanifu wa Mafunzo ya Vijana Walio nje ya Shule.Picha zote na Benjamin Sawe