Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari(Hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kushuka kwa mfumuko wa bei kwa Machi mwaka huu. Kulia ni Meneja wa Ajira na Bei wa NBS, Ruth Minja.
Kulia ni Meneja wa Ajira na Bei wa NBS, Ruth Minja akiwa kwenye mkutano wa waandishi wa habari na Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo jijini Dar es Salaam leo.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
MFUMUKO wa Bei kwa Machi 2016 umepungua hadi asilimia 5.4 kutoka asilimia 5.6 ya Februari.
Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo amesema kuwa upandaji wa bei za bidhaa kwa mwaka ulioshia kwa Machi , 2016 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioshia Februari mwaka huu.
Amesema Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 101.93 mwenzi Machi, 2016 kutoka 96.69 mwezi Machi 2015.
Kwesigabo amesema kuwa mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mweziMachi, 2016 umepungua hadi asilimia 8.5 kutoka 9.5 iliyokuwa kwa Februari, 2016.
Amesema kupungua kwa mfumuko wa bei wa mwezi Machi, 2016 kumechangiwa hasa na kupungua kwa bei za bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Machi 2016 zikilinganishwa na bei za mwezi Machi 2015.
Kwesigabo amesema mwenendo wa bei za bidhaa zisizo za vyakula zinaonyeshwa kupungua kwa mwezi Machi 2016 ikilinganishwa na mwezi Machi 2015 bidhaa hizo ni Gesi asilimia 10, Diseli 5.8, Mafuta 1.0.
Mfumko wa bei unafanana nchi za Afrika Mashariki , kwa mwezi Machi nchi ya Kenya Mfumuko umepungua hadi asilimia 6.45 kutoka asilimia 6.8 kwa Februari, Uganda mfumuko wa bei umepungua hadi asilimia 6.2 kwa Machi 2016 kutoka asilimia 7.0 kwa Februari 2016.