Saturday, September 27, 2014

NSSF YAWATEMBEZA WAHARIRI KUONA MIRADI MIKUBWA DAR ES SALAAM



NSSF YAWATEMBEZA WAHARIRI KUONA MIRADI MIKUBWA DAR ES SALAAM
 Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la kisasa la Kigamboni, kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi Karrim Mataka (kulia), akitoa maelezo ya mradi ujenzi wa daraja hilo kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari, wanaotembelea mradi mbalimbali ya uwekezaji unaofanywa na NSSF. Wa pili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Creasentius Magori.
 Wahariri wa Vyombo vya Habari, wakijaribu kupita kwenye njia ya dharura, kwa ajili ya kuangalia mradi mkubwa wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, unaofanywa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
 Wahariri wa Vyombo vya Habari, wakimsikiliza kwa makini, Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la kisasa la Kigamboni, kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi Karrim Mataka (mwenye koti kulia), wakati akitoa maelezo ya mradi ujenzi wa daraja hilo, wakati wahariri hao, walipotembelea miradi mbalimbali ya uwekezaji inayofanywa na NSSF. Wa tatu kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Cresentius Magori. 
 Wahariri wa Vyombo vya Habari wakimshuhudia Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Cresentius Magori, akipita kwenye kwenye kivuko cha muda, wakati wakitoka kuangalia mradi mkubwa wa Ujenzi wa daraja la kisasa la Kigamboni, Dar es Salaam jana.
 Wahariri wa Vyombo vya Habari, wakimsikiliza kwa makini, Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la kisasa la Kigamboni, kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi Karrim Mataka (mwenye koti), wakati akitoa maelezo ya ujenzi wa daraja hilo, wakati wahariri walipotembelea miradi mbalimbali ya uwekezaji inayofanywa na NSSF.
 Wahariri wa Vyombo vya Habari wakipita kwenye daraja la muda, lililojengwa kwa ajili ya kupitisha vifaa vya ujenzi, walipofanya ziara ya kuangalia miradi mikubwa ya uwekezaji inayofanywa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dar es Salaam jana.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Cresentius Magori, akijibu maswali ya Wahariri wa Vyombo vya Habari, walipotembelea mradi mkubwa wa uwekezaji katika Kijiji cha DEGE Eco, Kigamboni, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha, Lodovick Mroso na Meneja Kiongozi wa Mahusiano na Huduma kwa Wateja, Eunice Chiume.