Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (Mbeya University of Science and Technology-MUST) (Chancellor),Profesa Mark Mwandosya (kulia) akiwa kwenye mkutano na uongozi wa Chuo hicho ofisini kwake Ikulu,Dar es Salaam.Ujumbe huo,ukiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo umempa taarifa Mkuu wa Chuo kuhusu maendeleo ya Chuo, changamoto zinzokikabili,na mipango ya kukiimarisha Chuo kifedha,kitaaluma,na miundombinu yake.
Mkuu wa Chuo hicho,Profesa Mark Mwandosya,ambaye pia ni Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais(Kazi Maalum),wa kwanza kulia mstari wa mbele; akiwa na Profesa Penina Mlama, Mwenyekiti wa Baraza,katikati; na Profesa Joseph Msambichaka,Makamu Mkuu wa Chuo akiwa wa kwanza kushoto.Walio mstari wa nyuma kutoka kushoto ni Profesa Emmanuel Lwoga, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo mwenye dhamana ya mipango na fedha, Ndugu Augustine Olga, Makamu Mwenyekiti wa Baraza, na Profesa Osmund Kaunde, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo mwenye dhamana ya taaluma.