Meya wa Manispaa ya Ilala, Mstahiki Meya Jerry Silaa leo aliandaa futari iliyohudhuriwa na watu mbalimbali wakiwepo viongozi wa dini, viongozi wa serikali, madiwani, wafanyabiashara na wananchi wa kawaida na kufanyika katika ukumbi wa jiji wa Anatoglo Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Pichani ni Meya Slaa akigawa tende kwa watu waliofunga.
Mustapher Hassanali akiongoza wafanyakazi wa 361 kuandaa zawadi kwa wageni waalikwa. kampuni hiyo ndio iliyoratibu shughuli nzima ya kufuturisha.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akimkaribisha Dr. Reginald Mengi katika futari hiyo.
Dr. Reginald Mengi akisalimiana na SHEIKH Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akiwakaribisha wananchi waliohudhuria futari hiyo aliyowandalia.
Waumini wakiwa katika swala.
Wageni waalikwa wakipakua futari iliyoandaliwa na Meya wa Manispaa ya Ilala.
Viongozi mbalimbali wakifuturu.
SHEIKH Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum, akitoa neno la shukrani kwa niaba ya waalikwa wote.
Mstahiki Meya, Jerry Silaa akizungumza wakati wa kufuturisha.
Duaa ilisomwa na SHEIKH Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum, huku Mstahiki Meya Jerry Silaa akiipokea.
Mstahiki Meya akitoa zawadi kwa wageni mbalimbali waalikwa.
Mstahiki Meya wa Manipaa ya Ilala, Jerry Silaa (kanzu nyeupe) akipiga picha ya pamoja na vijana wa 361 waliofanikisha shughuli hiyo ya kufuturisha.