Na              Daudi Manongi-MAELEZO
        Katibu                Mkuu Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Prof Adolph                Mkenda amesema kuwa serikali imeondoa tozo ya uhakiki wa                viwango vya ubora na usajili katika kuanzisha viwanda                vidogovidogo katika shirika la viwango Tanzania                Tanzania(TBS) ambao sasa unafanyika bure.
        Prof                Mkenda ameyasema hayo alipokuwa akitoa mada katika                uzinduzi wa Jukwaa la kuwezesha wanawake na akaunti ya                mkopo ya MALAIKA ambayo imeanzishwa katika benki ya                Wanawake Tanzania.
        Aidha                amesema ameagiza kwa wilaya na vijiji kuanzisha viwanda                kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanaunga mkono jitihada                za serikali ya awamu ya Tano na kuinua uchumi wa nchi                yetu."Bidhaa za kilimo kwa sasa zinapewa              dhamana na hivyo basi nawaimiza wanawake waanzE kuanzisha              viwanda vidogovidogo kwani uanzishwaji wake ni bure."Alisema              Prof Mkenda.
        Pia                alisema kuwa kipato cha kati nchini kinaongezeka siku hadi                siku na kuwataka wanawake kutolima kwa mazoea na kuwataka                wafanye biashara kwa faida kwa kutumia teknolojia sahihi                ili kuongeza uzalishaji.
        Katika                upande mwingine aliwataka wanawake kutokata tamaa katika                kujiinua kiuchumi kwani Serikali ya awamu ya tano iko                makini na inaweka mazingira mazuri kwa wanawake kama                kuondoa tozo zisizokuwa za lazima ili kuvutia wawekezaji                wa viwanda vidogo vidogo.
        Katika                uzinduzi huo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa                Tanzania Bi Samia Suluhu Hassan alizindua jukwaa hilo na                akaunti ya mikopo ya wanawake ya MALAIKA kupitia benki ya                wanawake ambayo akaunti hiyo itakuwa na mikopo yenye riba                nafuu ya asilimia 5 kwa muda wa miezi sita,mafunzo                yanatolewa bure,hamna haja ya kuleta mchanganuo wa                mahesabu na hakuna hitaji la dhamana yenye lengo la                kuwakwamua wanawake kiuchumi.