Thursday, May 22, 2014

NMB MBEYA YAKABIDHI MSAADA KWA MBUNGE WA VITI MAALUMU MKOA WA MBEYA.

 
 
 
 
 
 
Meneja wa NMB Kanda Lecrisia Makiriye (Kulia) Akikabidhi Msaada wa Madawati kwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya Dk. Mary Mwanjelwa ambaye pia ni M-NEC Taifa kupitia Chama cha Mapinduzi CCM
 
Meneja wa NMB Kanda Lecrisia Makiriye (Kulia) Akikabidhi Msaada wa  Mashuka  kwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya Dk. Mary Mwanjelwa ambaye pia ni M-NEC Taifa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM)
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. Mary Mwanjelwa ambaye pia ni M-NEC Taifa akimshukuru  Meneja wa NMB Kanda Lecrisia Makiriye baada ya kupokea misaada hiyo
 
***
BENKI ya Nmb Kanda ya Nyanda za Juu Kusini imekabidhi msaada wa Madawati na mashuka vyenye thamani ya Shilingi Milion 10 kwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya(CCM) Dk. Mary Mwanjelwa.
 
Msaada huo ni pamoja na madawati 83 na mashuka 250 ambavyo Mbunge huyo alikabidhiwa na Meneja wa Kanda wa NMB katika hafla iliyofanyika katika ofisi za Benki hiyo zilizopo Mbalizi Road jijini Mbeya.
 
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Meneja wa NMB Kanda, Lecrisia Makiriye, alisema benki ya NMB inatoa huduma zake katika jamii ya watu mbali mbali kwa kuwa ndiyo wadau wanaofanya Benki hiyo kupata maendeleo.
 
Alisema wanajamii hao ambao ndiyo wateja wao wanakumbana na changamoto mbali mbali ambazo zinawazunguka hivyo kama wadau wa Serikali hawana budi kujitokeza na kutoa msaada pale inapotokea.
 
Alisema katika msaada wa leo Benki hiyo imetoa mashuka 250 kwa ajili ya Hospitalini na Madawati 83 kwa ajili ya wanafunzi wa Shule za Msingi ndani ya Mkoa wa Mbeya ambao shule zao zinaupungufu wa madawati.
 
Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya(CCM),Dk. Mary Mwanjelwa, alisema kama Mbunge mwanamke anaguswa sana anapoona jamii inakumbwa na matatizo mbali mbali.
 
Alisema kutokana na jamii kuhitaji mahitaji makubwa akaona ni vema akaomba msaada kwa Benki ya NMB kwa ajili ya kusaidia wenye shida ambapo Benki hiyo imesikia kilio chake na kutoa msaada huo kutokana na alivyoomba.
 
Alisema sehemu ya mashuka hayo Mashuka 100 atapeleka kwa waliokumbwa na mafuriko hivi karibuni wilayani Kyela na mashuka mengine 150 atapeleka kwa wagonjwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya.
 
Alisema Madawati atayagawa katika Shule za Msingi zenye upungufu ndani ya Mkoa wa Mbeya kadri itakavyowezekana kutokana na mahitaji ya madawati kuwa bado makubwa katika kuinua kiwango cha Elimu mkoani Mbeya.
 
Aidha alitoa wito kwa taasisi na watu binafsi kuendelea kujitolea kwa msaada wa hali na mali kwa wananchi wa Wilaya ya Kyela kutokana na mafuriko yaliyowakuta kwamba bado hali zao hazijatengemaa hivyo jitihada zaidi zinahitajika.
 
Alisema katika kuonesha wananchi wa Kyela wanahitaji bado misaada pia Wabunge wa Mkoa wa Mbeya wanajipanga kuhakikisha wanatoa chochote kwa ajili ya kuwasaidia wananchi waliokumbwa na mafuriko.

Na Mbeya yetu