Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imemuhukumu mwalimu mstaafu wa Shule ya Msingi Mpanda Ndogo Wilayaya ya Mpanda Rashid Mbogo kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mjukuu wake (5) na kumuharibu vibaya sehemu zake za siri
Hukumu hiyo ilisomwa hapo leo na Hakimu Mkazi mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa baada ya mahakama kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na pande zote mbili za mashitaka na utetezi
Awali katika kesi hiyo mwendesha mashitaka Godfrey Rwezabila alidai mahakamani kuwa mshitakiwa Rashid Mbogo alitenda kosa hilo oktoba 19 mwaka jana majira ya saa mbili na nusu usiku nyumbani kwake huko katika Kijiji cha majalila Wilayani hapa
Siku hiyo ya tukio mshitakiwa alidaiwa kumbaka mjuu kuu wake huyo wakati akiwa amelala chumbani kwenye godoro wakati akiwa amelala na mtoto wake na Rashid Mbogo aitwaye Faraji Mbogo(9) ambae alishuhudia wakati baba yake akimbaka mtoto huyo
Ilielezwa mahakamani na mwendesha mashitaka kuwa siku hiyo mke wa mshitakiwa alimuuga mume wake kuwa anakwenda kwenye zizi la mbuzi lililokuwa jirani na nyumbani kwao kufungia mbuzi ndipo alipotumia nafasi hiyo ya kuingia chumbani na kumkuta mjuu kuu wake akiwa amelala na mtoto wake na kisha alimshika na kuanza kumbaka huku mtoto wake wa kuzaa mwenyewe akiwa anashudia tendo hilo
Alieleza mshitakiwa aliweza kukamatwa siku hiyo hiyo na majirani zake ambao walimpeleka hadi kituo cha polisi cha Wilaya ya Mpanda huku mjukuu wake nae alikimbizwa kwenye hospitali ya Wilaya ya Mpanda kwa ajiri ya kupatiwa matibabu baada ya kuwa ameharibiwa vibaya kwenye sehemu zake za siri
Mshitakiwa katika utetezi wake ambapo hakuna na shahidi hata mmoja huku upande wa mashitaka ukiwa na mashahidi sita akiwepo mtoto wake mwenyewe Faraji Mbogo alikana kutenda kosa hilo kabisa kwalealicodai mahakamani hapo kuwa umri wake ni mkubwa na kwa sasa ameishaishiwa nguvu za kiume hivyo asingetenda kosa hilo
Baada ya utetezi huu mahakama iliamuru mshitakiwa akapimwe hospitalini ili baini kama kweli hana nguvu za kiume ambapo majibu ya daktari yalionyesha kuwa Rashid Mbogo bado anazo mbegu za kiume zinazomfanya atende tendo la ndoa
Hakimu Chiganga baada ya kurudhika na ushahidi uliotolewa aliiambia mahakama kuwa mshitakiwa amepatikana na kosa la kifungu cha sheria namba 130 na 131 cha marekebisho ya sheria ya mwaka 2009
Akisoma hukumu hiyo alisema kutokana na kuapatikana na kosa hilo bila mashaka yoyote mahakama imemuhukumu Rashid Mbogo kutumikia kifungo cha maisha jela
Na Walter Mguluchuma
Katavi