Tuesday, June 30, 2015

WATATU WATIWA MBARONI JIJII DAR ES SALAAM KWA TUHUMA ZA MAUAJI



WATATU WATIWA MBARONI JIJII DAR ES SALAAM KWA TUHUMA ZA MAUAJI























Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji ya mmiliki wa shule ya Mtakatifu Zion iliyopo  maeneo ya Ununio, Mbezi Beach wilaya ya kipolisi Kawe mkoa wa kipolisi wa Kinondoni aliyejulikana kwa jina la ANNA D/O MIZINGI, Miaka 48, Mfanyabiashara, Mkazi wa Boko.



Mnamo tarehe 02/02/2015 majira ya saa za mchana mtoa taarifa alifika kituo cha Polisi na kueleza kwamba marehemu ANNA D/O MIZINGI aliondoka tangu tarehe 26/12/2014 majira ya saa 1:00hrs akiwa na mmoja wa watuhumiwa wakitumia gari dogo aina ya Toyota Verosa ambayo namba zake hazikufahamika mara moja iliyokuwa inamilikiwa na marehemu na tangu wakati huo hakuwa ameonekana tena.

Kutokana na taarifa hizo Jeshi la Polisi lilifungua jalada la uchunguzi na kuanza uchunguzi mara moja. Wakati uchunguzi ukiendelea zilipatikana taarifa zilizosaidia kukamatwa kwa watuhumiwa hao huko Uchira Miwaleni, Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

Watuhumiwa walipokamatwa na kuhojiwa mtuhumiwa mmoja kati ya hao watatu amekiri na kutoa maelezo kuwa siku ya tukio aliondoka na marehemu kuelekea katika shule ya Mt. Zion. Kwamba walipofika shuleni hapo walivamiwa na watu wapatao wanne na kuanza kupigwa lakini yeye alifanikiwa kutoroka na kujificha katika uzio wa shule hiyo. Amesema akiwa katika uzio huo aliwaona watu hao wakiendelea kumpiga marehemu ANNA D/O MIZINGI na kisha kumtupa katika shimo la choo. Baada ya kitendo hicho watu waliotenda uhalifu huo waliondoka na gari la marehemu na kutokomea kusikojulikana.

KWA HISNI YA MICHUZI BLOG