Sunday, December 07, 2014

JK afanya Kisomo Kumshukuru Mwenyezi Mungu Kwa Kupona



JK afanya Kisomo Kumshukuru Mwenyezi Mungu Kwa Kupona
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia  Mashekhe na wageni waliohudhuria hafla ya kisomo maalum cha Kumshukuru Mwenyezi Mungu baada ya kufanyiwa upasuaji na kurejea nyumbani salama kilichofanyika katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam leo.
 Mjukuu wa Rais,  Ayman Ridhiwani Kikwete akicheza kwa furaha wakati Babu yake Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwashukuru wageni na Mashekhe waliohudhuria hafla ya kisomo maalum kilichofanyika katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam leo
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea katika hafla ya kisomo maalum cha Kumshukuru Mwenyezi Mungu baada ya kufanyiwa upasuaji na kurejea nyumbani salama kilichofanyika katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa  na mjukuu wake Ayman Ridhiwani Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kumalizika kisomo cha shukran kwa Mwenyezi Mungu kiklichofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo. Picha na Freddy Maro