Na Sultani Kipingo
Taasisi za serikali, mashirika ya umma wizara na idara mbalimbali za serikali zimeshauriwa kushiriki katika mashindano ya uwasilishaji wa taarifa bora za fedha za mwaka tofauti na ilivyo sasa ambapo makundi haya yamekuwa yakishiriki kwa uchache sana na sehemu kubwa ya washiriki kuachiwa taasisi na mashirika binafsi.
Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji tuzo na vyeti kwa washindi katika uwasilishaji wa taarifa bora za fedha mwaka 2014, Naibu Waziri wa Fedha, Mhe Adamu Malima amesema ni wakati mwafaka kwa taasisi na idara mbalimbali za serikali kuingia katika mashindano hayo ili kujipima na kuongeza ufanisi katika utunzaji na uandaaji wa taarifa zao kulingana na viwango vya kimataifa IFRS.
Katika mshindano hayo ambayo huratibiwa na bodi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu nchini NBAA kwa mwaka huu jumla ya washiriki 40 walishiriki ambapo mamlaka ya mapato nchini TRA Iliibuka mshindi wa kwanza kwa uwasilishaji wa taarifa bora za fedha kwa mwaka 2013 -2014. kwa upande wa taasisi za serikali.
Kamishna Mkuu wa TRA Rished Bade akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokea tuzo za kuweka mahesabu vizuri kwa taasisi bora za serikali mwaka 2013-2014 iliyotolewa NBAA.
Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima (kushoto) akimkabidhi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Rished Bade Ngao ya ushindi wa kwanza kwa taasisi za serikali kwa kuweka kumbukumbu za mahesabu vizuri mwaka 2013/14 inayotambuliwa na Bodi ya Wakaguzi wa Mahesabu nchini (NBAA), juzi mkoani Arusha, wanaoshudia ni wafanyakazi wa TRA.
Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima akifurahia jambo na Kamishna Mkuu wa TRA Rished Bade.
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi pamoja na viongozi na watumishi wa TRA.
Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima akifurahia jambo na Kamishna Mkuu wa TRA Rished Bade.
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi pamoja na viongozi na watumishi wa TRA.