Sunday, December 07, 2014

Mahafali ya tano ya chuo kikuu cha St. John's mjini Dodoma yafana



Mkuu wa chuo kikuu kikuu cha St, John Askofu Donald d Mtetemela katikati akiwa na viongozi wa kanisa la anglikan ambalo ndilo mmiliki wa chuo hicho walipokuwa kwenye mahafali ya tano ya chuo hicho.
 Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Philip Alfred aliyekuwa Mgeni Rasmi kwenye mahafali ya tano ya wanafunzi wa chuo kikuu cha St, John's cha mjini Dodoma akihuwahutubia wahitimu wa kozi mbalimbali wa chuo hicho.
 Mkuu wa Skuli za kidini akihutubia jambo kwenye mahafali hayo.
Wahitimu wa Shahada ya sayansi katika uuguzi wakila kiapo cha utumishi uliotukuka wakati wa mahafali ya tano ya chuo kikuu cha St, John's kinachomilikiwa na kanisa la anglican kilichopo mjini Dodoma
Meneja wa CRDB Tawi la Dodoma Bi Rehema Hamisi akiwa na mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 kwa ajili ya kukabidhi kwa viongozi wa chuo kikuu cha st, John's kama mchango wa maendeleo ya chuo hicho
 
 Kushoto mkurugenzi wa Wateja wakubwa, Taasisi na mashirika wa benki ya CRDB Philip Alfred akiwakabidhi viongozi wa chuo kikuu cha Mtakatifu Yohana (St, John's) cha mjini Dodoma Mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya chuo hicho kilichopo chini ya kanisa la anglican Tanzania
   Wahitimu wa kozi mbalimbali za chuo kikuu cha St, John's wakiwa katika mahafali ya tano ya chuo hicho yaliyofanyika mjini Dodoma.
Baadhi ya wandishi wa habari mjini Dodoma wakimpongeza kwa kumpa maua mwandishi wa gazeti la mwananchi mkoani humo Israel Mgusi baada ya kuhitimu shada ya theogia na Elimu ya chuo kikuu cha St, John's

NA JOHN BANDA, DODOMA

IMEELEZWA kuwa watu mbalimbali wakiwemo wasomi wamekuwa wakiishi maisha ya anasa kubwa katika jamii huku wakiwa hawajulikani kazi wanazofanya hali inayolifanya taifa kuchelewa kupiga hatua
kimaendeleo. Kauli hiyo imetolewa na mkurugenzi wa wateja wakubwa, taasisi na mashirika wa Benki ya CRDB Fhilip Alfered wakati akiongea na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha mtakatifu Yohana (ST. John's) kilichopo mjini
Dodoma kwenye mahafali ya tano yaliyohusisha wanafunzi 1608 waliohitimu katika kozi mbalimbali.
Mkurugenzi huyo alisema tatizo kubwa lililopo miongoni mwa vijana na hata waomi ni kutawaliwa na hisia potofu kuwa njia za kuweza kufanikiwa kiurahisi katika maisha ni  utapeli, ujanjaujanja na za mkato, kibaya zaidi ni jamii kuwa tabia ya kusifia na kuenzi mafanikio mafaniao yanayotokana na njia hizo.
Alfred alisema siku hizi kuna watu wanaitwa mission town [magumashi] ni vijana ambao hawajulikani wanafanya shughuli gani laki huonekana kuwa na vipato vikubwa huku wakiishi maisha ya kifahari yaliyojaa anasa na cha kushangaza na kusikitisha ni jinsi jamii hasa vijana wanapowatukuza na kuwahusudu watu hawa bila kujali wali kuhoji vyanzo halisi vya vipato vyao.
Alisema kama hilo halitoshi vijana wanapoajiliwa hasa katika maeneo ya benki ni kufanya njama za kuiba mamilioni wenyewe wanaita kupiga dili na hali hiyo ipo kila mahali wanapoajiliwa kwa ajili ya kutoa haki wao wanfikilia namna ya kupata rushwa kiurahisi. '' nawatahadhalisha kuwa njia hizo pamoja na kuwa si tu siyo  endelevu lakini pia huwapotosha vijana wengi kujiingiza kwenye vitendo viovu kama vile ujambazi, wizi, wizi wa kalamu, utapeli ngono, ngono nzembe kutumia au kuuza madawa ya kulevya ambavyo matokeo yake sisi sote
tunayafahamu siyo mazuri,
'' napenda kuwaasa kuwa njia ya pekee na endelevu itakayowaletea maisha bora ni ile mliyoichagua ya kujipatia elimu inayoambatana na maadili mema, anayetumia elimu yake kutenda maovu hatasamehewa na jamii bali atakaetenda mema ataenziwa vizazi na vizazi nawasihi mchague kutenda mema'', alisema
Aidha Mkurugenzi huyo alikabidhi hundi ya tsh 10 mil kama mchango kwa chuo hicho huku akiahidi kutoa mkopo ili kukiwezesha chuo hicho kujitanua zaidi.
Awali naibu mkuu wa chuo cha ST JOHN'S  alisema Pro. Emmanuel Mbennah alisema chuo hicho ili kiweze kujitanua na kutoa huduma ipasavyo itawaghalimu 5.6 bilion ambapo ujenzi wa mabweni ya wanafunzi utaghalimu 3,6 bilion na ujenzi wa jingo la taaluma itakuwa 2. Billion huku chuo hicho kikiwa na matawi yaki Kigoma na Dar es laam.