Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisisitiza jambo baada ya kupata maelezo juu ya maendeleo ya Mradi wa Daraja la Kigamboni kabla ya kufanya ziara ya siku moja ya kutembelea Miradi iliyofadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadani Dau (kushoto) akitoa maelezo juu ya miradi ujenzi wa kijiji cha kisasa kiitwayo 'Dege Eco Village modern city Housing scheme' yenye thamani ya matrilioni. Waziri Mkuu Mizengo Pinda alikuwa na ziara ya siku moja ya kutembelea miradi mikubwa ya miundombinu ya mfuko huo jijini Dar es Salaam.
Msimamizi wa Mradi wa ujenzi wa Daraja la Kigamboni Mhandisi Karim Mattaka (kulia) akimuonyesha Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wapili kulia) mchoro sanifu wa daraja la Kigamboni, wakati wa ziara ya waziri mkuu kutembelea miradi mitatu mikubwa inayofadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) jijini Dar es Salaam.
Msimamizi wa Mradi wa ujenzi wa Daraja la Kigamboni Mhandisi Karim Mattaka (kulia) akimuonyesha Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wapili kulia) hatua za ujenzi wa daraja la Kigamboni, wakati wa ziara ya waziri mkuu kutembelea miradi mitatu mikubwa inayofadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wapili kulia) akitembelea mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni unaofadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakati wa ziara yake ya siku kutembelea miradi mitatu mikubwa inayofadhiliwa na NSSF jijini Dar es Salaam Jumamosi.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (Watano Kulia) katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali na wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) mara baada ya kutembelea mradi wa daraja la Kigamboni ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku moja ya kutembelea miradi mitatu mikubwa inayofadhiliwa na NSSF jijini Dar es Salaam Jumamosi.