Sunday, April 05, 2015

WAZIRI MKUU, MIZENGO PINDA AFIWA NA MKWEWE



WAZIRI MKUU, MIZENGO PINDA AFIWA NA MKWEWE
Spika wa Bunge Anne Makinda akitoa pole kwa familia ya Marehemu akiwemo mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (kulia) ambaye alifiwa na baba yake Mzazi, Mzee Abdallah Rehani , Nyumbani kwa marehemu,Tabata jijini Dar es salaam Aprili 4, 2015 . Wengine pichani ni ndugu wa karibu wa Mama Pinda.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa katika mazishi ya babamkwe wake yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Segerea jijini Dar es salaam Aprili 4, 2015. Kushoto ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad.
Waombolezaji wakisoma dua ya kumwombea marehemu Abdallah Rehani, Baba Mzazi wa Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda, Marehemu Mzee Abdallah Rehani nyumbani kwa Marehemu, Tabata jijini Dar es salaam Aprili 4, 2015.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi akimpa pole Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika mazishi ya baba mzazi wa mkewe, Marehemu Mzee Abdallah Rehani yaliyofanyika kwenye makaburi ya Segerea jijini Dar es salaam, Aprili4, 2015.
Waombolezaji wakizika mwili wa baba mzazi wa mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda , Marehemu Abdallah Rehani kwenye Makaburi ya Segerea jijini Dar es salaam, Aprili 4, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akishiriki katika mazishi ya Baba Mkwe wake , Marehemu Abdallah Rehani kwenye makaburi ya Segerea jijini Dar es salaam Aprili 4, 2015.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad akishiriki katika mazishi ya Baba mzazi wa Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda, Marehemu Abdallah Rehani kwenye makaburi ya Segerea jijini Dar es salaam Aprili 4, 2015.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi akishiriki katika mazishi ya Baba mzazi wa Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda, Marehemu Abdallah Rehani kwenye makaburi ya Segerea jijini Dar es salaam Aprili 4, 2015.
Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dr. Wilbroad Slaa akishiriki katika mazishi ya baba mzazi wa Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda, Marehemu Abdallah Rehani yaliyofanyika kwenye makaburi ya Segerea jijini Dar es salaam Aorili 4, 2015.
Baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Siasa na Serikali walioshiriki katika mazishi ya Baba Mzazi wa Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda, Marehemu Abdallah Rehani yaliyofanyika kwenye makaburi ya Segerea jijini Dar es salaam Aprili 4, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Makamu wa Kwanza wa rais wa Zanziba Seif Sharif Hamad wakitoka kwenye eneo la makaburi ya Segerea jijini Dar es salaam baada ya mazishi ya baba mzazi wa Mke wa Waziri Mkuu, Marehemu Abdallah Rehani Aprili 4, 2015. Kushoto ni Waziri Mkuu, Mstaafu, Frederick Sumaye na mwenye koti jeusi katikati ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi.(Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu)