Ndege kubwa ya kwanza ya shirika                la ndege la Serbia, Airbus A330, ikiwa katika uwanja wa                ndege wa Nikola Tesla. Ndege hii itakuwa ikifanya safari                zake kati ya Belgrade na New York.
        Shirika la ndege la Serbia, ambalo                ni shirika la ndege la Taifa la Serbia, lilisherehekea                hatua nyingine katika mabadiliko kama shirika la ndege                linaloongoza katika kanda, kwa kuwasili kwa ndege yake                kubwa ya kwanza katika uwanja wa ndege wa Nikola Tesla                jana.
        Ndege aina ya Airbus A330                itatumika katika ruti za shirika la ndege la Serbia kati                ya Belgrade kwenda New York, Ambayo itazinduliwa tarehe 26                Juni 2016, ikiunganisha Serbia na Marekani kwa huduma ya                ndege ya moja kwa moja kwa mara ya kwanza katika miaka 24.
        Baada ya kutua Belgrade, ndege                hiyo ililakiwa kwa salamu za kitamaduni za urushaji wa                maji na kukabidhiwa kwa wawakilishi wa ndege hiyo.                Waliokuwa katika safari ya kwanza ya ndege hiyo ya                kihistoria ni kundi la wadau wakubwa wakiongozwa na Siniša                Mali, Mwenyekiti wa shirika la ndege la Serbia na Meya wa                Belgrade, na Dane Kondić, Mkurugenzi mkuu wa shirika la                ndege la Serbia.
        Ndege hiyo ilikuwa inaongonzwa na                Kaptein Davor Mišeljić, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la                ndege la Serbia, na sasa itasajiliwa na Idara ya                Usafirishaji na Uchukuzi ya Serbia (Serbian Civil Aviation                Directorate) kabla ya kurejea tena Abu Dhabi kwa ajili ya                kukamilisha sehemu za vyumba vya ndege hiyo.
        Bwana Mali alisema: "Hii ni hatua                kubwa sana kwa shirika la ndege la Serbia na taifa kwa                ujumla. Kutazama ndege yetu ya kwanza iliyochorwa picha                isemayo Airbus A330 ikitua katika kiwanja chake kipya hapa                Belgrade kwa mara yake ya kwanza ilikuwa ni wasaa wa                faraja kwetu, kuona kuwa Ndege kubwa inakuja kuwekeza                katika hatma ya shirika hili la ndege na taifa la Serbia                pia.
        "Ndege yetu kubwa kabisa na ndege                zetu nyingine kubwa za A319, A320, ndege na A330 ni                uwekezaji ulio bora zaidi ambao utaiunganisha Serbia na                Marekani katika wiki chache itafungua utalii na biashara                kwa ajili ya uchumi."
        Ndege hiyo ina viti 18 katika                Daraja la biashara na viti 236 katika daraja la uchumi.                Ndege hiyo Aina ya Airbus A330 itafanya safari zake katika                safari tano mpya za kila wiki za shirika la ndege la                Serbia kati ya Belgrade na New York.
        Kuwasili kwa A330 ni hatua mpya                kabisa katika hatua za msingi za programu ya kuongeza                ndege (re-feeling) ambayo ilianza mwaka 2013 na imekuwa ni                kitambulishi cha ndege kumi za kawaida katika miaka kumi                tu iliyopita, ikipunguza wastani wa umri wake wa ndege                zake kutoka miaka 25 hadi miaka 10.
         Bwana Kondic alisema: Kuwasili                kwa ndege aina ya Air bus A330 mchana wa leo lilikuwa ni                tukio la kihistoria kwa shirika la ndege la Serbia na                ishara ya mafanikio katika siku za usoni.
        "Ndege aina ya A330 ni ya kisasa                na inatumia mafuta vizuri ambayo inafungua fursa nyingi za                kukua kwa shirika la ndege na itaturuhusu kuzindua huduma                za muda mrefu kwenda New York, inarahisisha safari kwa                kiasi kikubwa huku ikiwezesha muunganiko kati ya Balkans                na Marekani.
        "Katika wiki zijazo ndege itakuwa                tayari ikiwa na madaraja mawili ya Business na Economy                ambayo zikiambatana na huduma zetu nzuri tunazotoa,                itawapatia wageni wetu uzoefu wa safari usiolinganishwa                kupitia Atlantic."
        Dondoo za huduma na bidhaa za                ndege ya A330 inajumuisha mfumo wa burudani katika kila                kiti inayokuwezesha kuchagua filamu, Muvi na burudani za                Kiserbia na Kiingereza, viti vya kulala katika daraja la                biashara na Menyu iliyoboreshwa, ikijumuisha huduma ya                chakula pale unapohitaji kwa wageni wa daraja la Business.
        