Wednesday, May 18, 2016

MKUU WA WILAYA YA BUKOMBE APIGA MARUFUKU MAANDAMANO YA WALIMU



MKUU WA WILAYA YA BUKOMBE APIGA MARUFUKU MAANDAMANO YA WALIMU
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya anapenda kuwatangazia Wananchi wa Bukombe na umma wote kwa ujumla kuwa maandamano yaliyoitishwa na Chama cha Walimu Wilayani hapa ambayo yanatarajiwa kufanyika tarehe 18/05/2016 ni batili na hayana msingi wowote kwani hoja zote 17 ambazo waliziorodhesha zilishajibiwa na Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Bukombe kupitia barua yenye Kumb. Na. A.30/3/84 ya tarehe 16/05/2016. 
 Aidha Mkuu wa Wilaya amekitaka chama cha Walimu kama hakikuridhishwa na majibu ya hoja zao, bado kina nafasi ya kukutana tena na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya na Kuzungumzia masuala hayo badala ya kufanya maandamano ambayo yataathiri shughuli za mitihani ya "Mock" kwa kidato cha nne iliyoanza tarehe 10 hadi 20/05/2015 na ile ya "STEP" chini ya BRN kwa shule za sekondari iliyoanza tarehe 16 hadi 20/05/2016. 
 Kamati kuu ya Ulinzi na usalama ipo imara kudhibiti maandamano hayo na vitendo vyovyote vinavyoashiria uvunjifu wa Amani katika Wilaya ya Bukombe. 

Imetolewa na:
 Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Bukombe
 Geita 
17 Mei, 2016