Sunday, April 05, 2015

SHIKA NDINGA WILAYA YA KINONDONI YAFANYIKA


SHIKA NDINGA WILAYA YA KINONDONI YAFANYIKA
Ndinga zinazoshndaniwa kwenye shindano la Shika Ndinga.
SHIKA ndinga ya EFM Radio kwa Wilaya ya Kinondoni imefanyika jana Aprili 5 mwaka huu katika Uwanja wa Garden Kinondoni jijini Dar es Salaam, ambapo wasikilizaji wa EFM waliopata nafasi ya kushiriki baada ya kujibu maswali mbalimbali kupitia vipindi vya redio walishindana kushika ndinga ya biashara.
Washiriki wa shindano kwa wanawake walikuwa 21 na wanaume 20 ambapo kati ya hao ni Wanawake watano na Wanaume watano tu waliofanikiwa kuendelea mbele katika raundi nyingine ambapo watashiriki katika fainali na washindi wengine kutoka katika Wilaya ya Ilala na Temeke.
Mtiririko wa kushika ndinga ulikuwa ni kusimama kwa miguu miwili huku washiriki wakiwa wameshika ndinga na baada ya kama dakika tano wanaume wengi walianza kushuka baada ya kushindwa kuhimili vigezo vilivyowekwa na wanawake walisimama imara kwa muda na baadaye nao walianza kushindwa kwa wingi kuliko wanaume.
Ndani ya saa la kwanza tu, washindi watano wanawake walipatikana hivyo zoezi hilo kubaki kwa wanaume, ambao baada ya muda kidogo walibadilishiwa zoezi la kushika ndinga kwa mguu mmoja na mwingine kuuinua usishuke chini hapo ndipo washindi watano Wanaume walivyopatikana.
Washindi kwa upande wa wanawake ni KHADIJA RASHIDI, SWAUMU IDDI, HAPPY AMBROS, NYABUHO PETER na  HABIBA huku kwa upande wa Wanaume ni ABDUL SAID, KASSIM SAID, ERNEST EDWARD, MUBARAK RAMADHANI pamoja na MBWANA KASANGA.