Monday, December 29, 2014

MBONI SHOW YA EATV YAHAMIA TBC



MBONI SHOW YA EATV YAHAMIA TBC
                                        Na Bakari  Issa,Dar es Salaam.

Mkurugenzi  wa Mboni  Show,Mboni Masimba  ameamua  kuhamishia kipindi  cha Mboni show katika kituo cha utangazaji  cha Taifa (TBC) kutoka EATV ili  kuvutia watazamaji wengi  na wapya kwa wazee pamoja  na vijana.

Kipindi  cha Mboni  Show  kitaanza kurushwa   TBC kuanzia  January  2 mwaka 2015 siku ya Ijumaa  saa 3 Usiku-4Usiku  na marudio  Jumanne  saa 9:00 mchana-10:00mchana.

Akizungumza  na waandishi wa  habari,mapema leo jijini Dar ndani ya ukumbi wa Idara ya Habari  (MAELEZO),Mboni  Masimba ametoa  shukrani  kwa EATV  kwa ushirikiano wao kwa kipindi  chote alichokuwa nao,na kusema kuwa amehamishia kipindi cha Mboni Show katika kituo cha TBC ili kuvutia watazamaji wengi hakuna atakaye tumia jina la Mboni  Show  na hakuna kitakachomkwamisha  kwa vile ana hati miliki.

"Nimeamia TBC kwa kuwa nahitaji  watazamaji wengi ,wote wazee na  vijana na hakuna atakaye tumia jina langu la Mboni  Show kwa kuwa nina hati miliki ya jina hili"alisema Mboni.

Kwa  upande  wake,Kaimu Mkurugenzi wa Masoko TBC,Bw.Fadhili  Chilumba amesema wamefurahi  kuwepo kwa Mboni  Show katika kituo cha Taifa(TBC) na kutoa wito kwa mashabiki kuweza kuwadhamini watu kama wakina Mboni  na wanamkaribisha sana. 


Nao  wadhamini wa Mboni  Show,Mfuko wa Taifa wa  Hifadhi ya Jamii (PSPF) wamesema wanamwezesha  Mboni  kuwepo  hewani  ili  kuhamasisha,kuelimisha  pamoja na kuburudisha umma wa Watanzania.