Friday, July 25, 2014

KUMBUKUMBU



KUMBUKUMBU
MAREHEMU MODEST SABINUS KWEKA.
14-04-1968 - 25-07-1999 

Ni miaka 15 leo,tokea ulipotuacha gafla baada ya kuitwa na Mungu Baba wa Mbinguni.Hatuna cha kusema ila ni kushukuru kwa kila jambo Mdogo wetu Modest, tokea hapo maisha ya Familia yetu hayajawa tena mazuri. machache Mungu alitukumbuka lakini kubwa kuliko yote, ni mama yako mzazi ambaye Kansa imemaliza sana, hana tena ziwa, Mguu mmoja na sasa tunakimbilia kukata wa pili. Tunaomba Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema atunusuru na janga hilo.

Unakumbukwa sana na Mkeo Mpenzi Constancia, Mwanao wa pekee Kelvin,Mama yako mzazi Ursula, Ndugu zako

Jane, Festo, Eugenia, Elizabeth, Cecilia, na Thadei;Mashemeji zako wote WaKweka wote wa Narumu, wa Wamallya na Manushi, Wafanyakazi wenzako wa Temeke Hospital wakazi wote wa Temeke Mikoroshini,Ndugu,Jamaa na Marafiki na wote waliokufahamu Misa ya Kumbukumbu Imesomwa mwanza leo Kanisa la Mt. Augustino – Mkolani Mwanza

"Lakini mtu mwema hata akifa kijana atapata pumziko………………………….huyo alionekana amempendeza Mungu, akapendwa naye, hata pindi alipokaa katikati ya wakosaji akachukuliwa.Naye akahamishwa ili uovu usimgeuzie nia yake, wala hila isimdanganye roha yake" Hek 4:7-11

"RAHA YA MILELE UMPE Ee BWANA"