Uongozi wa Tanzania Fellowship Churches unatarajia kufanya mkesha mkubwa kitaifa wa kuliombea Taifa,Desemba 31 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mkesha huo una lengo la kuliweka Taifa mbele ya usalama wa Mungu pamoja na kupatikana amani na utulivu kwa Taifa zima kwa ujumla.
Akithibitisha kuwepo kwa mkesha huo kitaifa,Mwenyekiti wa mkesha huo kitaifa,Mchungaji Geodfrey Mallasy amesema mkesha huo una lengo la kuliombea Taifa na kupatikana amani na utulivu.
"Mkesha huu una lengo la kuliweka Taifa letu mbele ya usalama wa Mungu na kuliombea Taifa letu amani na utulivu kutokana na bila amani hakuna kinachowezekana"alisema Mallasy.
Aidha,Mallasy ameeleza kuwa mkesha huo utahudhuliwa na mgeni rasmi ambaye ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Mohammed Gharib Bilal badala ya Rais Jakaya Kikwete kuomba radhi kutokana na tatizo la kiafya.
Hata hivyo,uongozi wa Tanzania Fellowship umeandaa usafiri kwa kampuni ya mabasi ya UDA kutoa huduma ya usafiri siku ya mkesha,pamoja na kutengeneza timu moja ya waimbaji,kukusanya sadaka zikazosaidia kuandaa mkesha mwingine utakaokuja