Monday, December 29, 2014

MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA KATA ZA MWENGE NA MATOPENI KATIKA WILAYA YA LINDI MJINI PIA AKUTANA NA NAIBU KATIBU MKUU WA CCM ZANZIBAR


MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA KATA ZA MWENGE NA MATOPENI KATIKA WILAYA YA LINDI MJINI PIA AKUTANA NA NAIBU KATIBU MKUU WA CCM ZANZIBAR
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi anayewakilisha Lindi Mjini na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Mwenyekiti wa CCM wa Tawi la Kilimahewa lililoko katika Kata ya Mwenge Ndugu Mohammed Madodo mara baada ya kuwasili katika Tawi hilo kwa ajili ya mkutano na viongozi wa Tawi tarehe 28,12.2014.
Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya Chama cha Mapinduzi anayewakilisha Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akihutubia wajumbe wa Halmashauri ya Tawi la Kilimahewa huko Lindi Mjini wakati wa ziara yake ya kuyatembelea matawi ya CCM wilayani humo tarehe 28.12.2014.
'Kitu hicho!……Chukua' Ndivyo alivyosikika akisema Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM Mama Salma Kikwete wakati alipokuwa akiongea na viongozi wa CCM wa Tawi la Kilimahewa .