Tuesday, November 04, 2014

JENGA TANZANIA FOUNDATION YAWALETEA KIPIMO CHA MALARIA PAPO HAPO !.


JENGA TANZANIA FOUNDATION YAWALETEA KIPIMO CHA MALARIA PAPO HAPO !.
Mwanadiaspora Mtanzania na Mkurugenzi wa JENGA TANZANIA FOUNDATION Bw. Nasoro Ally akitambulisha rasmi Home Malaria Kit katika mkutano wa  Africa Diaspora Market Place (ADMP III) uliofanyika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani tarehe 10/27/2014.
Akizungumza katika mkutano huo, Bw.. Nasoro Ally alieleza  kuwa  bado Malaria ni tishio kubwa la uhai kwa Sub-Sahara Africa na ni chanzo cha vifo vya watoto wadogo hasa chini ya umri wa miaka 5 . 
Kipimo hicho chenye uwezo wa kugundua vijidudu vya Malaria mwilini kati ya dakika 5 hadi 10 kimekubalika na shirika la World Health Organization (WHO) kama kipimo sahihi na cha haraka kwa upimaji wa Malaria nyumbani. Bw. Nassoro aliongeza kusema, kipimo hicho kitatolewa bure nchini Tanzania kwa familia zisizojiweza na kuhakikisha kinafika  sehemu mbali mbali za ndani hasa mikoani na vijijini ili kurahisisha upatikanaji wa huduma sahihi za afya na kufupisha safari ndefu na zenye milolongo.


Mkurugenzi wa JENGA TANZANIA foundation Bw. Nasoro Ally na Mwanasayansi msaidizi wa JENGA TANZANIA, Da. Asha Nyanganyi wakitambulisha rasmi kipimio cha nyumbani cha Malaria kwa  Mhe. Balozi Liberata Mumulala na wawakilishi wa USAID waliohudhuria mkutano huo.

VIDEO YENYE MAELEZO KUHUSU KIPIMO CHA NYUMBANI CHA MALARIA
Kipimo cha  Nyumbani cha Malaria Chenye Uwezo wa Kugundua Vijidudu  vya Malaria Vikiwemo Plasmodium Falciparim (PF) Vivax(PV)  Ovale (Po) na Malariae(Pm) antigen kati ya dakika 5 hadi 10 .


Mhe.Balozi Liberata Mulamula akipata kipimo cha  Malaria Mara moja kutoka kwa Mwanasayansi msaidizi wa JENGA  Asha Nyanganyi



Baadhi ya watu wachache walioshiriki katika kipimo hicho.

Shukrani; Images
Sunday Shomari
Jenga Tanzania Foundation
Story;
NesiWangublogspot.com