Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiwa na baadhi ya Wahitimu wa Kituo cha Chekechea cha Florence cha Kigogo Dar es salaam.
|
Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala akizungumza katika Mahafari ya Kituo cha Chekechea cha Florence yaliyofanyika Kigogo Dar es salaam. Watoto mia moja wamehitimu katika Kituo hicho na wote wamejifunza na kuelewa kusoma na kuandika. Balozi Kamala amewashukuru Bwana na Bibi Mbezi kwa kuanzisha kituo hicho. Aidha, Balozi Dr. Kamala ameanzisha mfuko wa zawadi wa Dr. Kamala "Dr. Kamala Award Fund" utakaokuwa unatoa zawadi kila mwaka kwa mtoto atakayeonesha kipaji cha uongozi. Baada ya Balozi Kamala kutoa laki moja za kuanzisha mfuko huo wazazi walimuunga mkono kwa kuchangia laki moja. Balozi Kamala amehaidi kuchangia milioni moja mfuko huo na riba itakayopatikana kila mwaka itatumika kutoa zawadi kwa mtoto atakayeonesha kipaji cha uongozi. Vile vile Balozi Kamala alichangia shilingi laki mbili na nusu kituo hicho na amehaidi kukitafutia wafadhili wa kukisaidia. |