Tuesday, August 19, 2014

Vodacom, FSDT yakutanisha wafanyabiashara na watoa huduma sekta ya fedha



Mkurugenzi wa Huduma za Uanachama wa Tanzania Private Sector Foundation (TPSF)Louis Accaro akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam(hawapo pichani) kuhusiana na warsha ya kuboresha na kupanua huduma za kifedha itakayofanyika kesho/leo Serena Hotel jijini Dar es Salaam, wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Mshauri wa TPSF Dk.Donath Olomi, Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia na Kulia ni Mtaalamu wa Biashara wa FSDT Peter Kingu,Warsha hiyo imedhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Mtaalamu wa Biashara wa Financial sector Deepening Trust(FSDT)akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusiana na warsha ya kuboresha na kupanua huduma za kifedha itakayofanyika kesho/leo Serena Hotel Dar es Salaam.Katikati ni Mkurugenzi wa Huduma za Uanachama wa Tanzania Private Sector Foundation (TPSF)Louis Accaro na kushoto ni Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia.Warsha hiyo inadhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Mkurugenzi wa Huduma za Uanachama wa Tanzania Private Sector Foundation (TPSF)Louis Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia, Mshauri wa TPSF Dk.Donath Olomi na Mtaalamu wa Biashara wa FSDT Peter Kingu(kulia) mara baada ya mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam(hawapo pichani) kuhusiana na warsha ya kuboresha na kupanua huduma za kifedha itakayofanyika kesho/leo Serena Hotel Dar es Salaam na kudhamiwa na Vodacom Tanzania.

Zaidi ya wafanyabiashara 100 wadogo na wa kati wanakutanishwa na watoa huduma sekta ya fedha kesho (Jumanne Agosti 19, 2014) jijini Dar es salaam katika semina maalum iliyoandaliwa na Taasisi ya sekta bianfsi Nchini (TPSF) iliyofadhiliwa na Vodacom na FSDT.

Mkutano huo unaofanyika chini ya ufadhili wa Kampuni ya Vodacom na Taasisi ya ukuzaji sekta ya fedha nchini (FSDT) unafanyika katika hoteli ya Serena chini ya Uenyekiti wa Mwenyekiti wa TPSF Dk. Reginald Mengi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Huduma za Uanachama wa TPSF Luis Akaro amesema shabaha ya  semina hiyo ni kujadili vikwazo vya upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wafanyabiashara  na kubadilishana uzoefu.

Amesema kumekuwepo na ukuaji mdogo wa biashara kutokana na ugumu wa upatikanaji wa mikopo hali inayochangia ukosefu wa ajira nchini na mchango wa nyanja hiyo katika ukuaji wa kasi wa uchumi wa nchi.

"Tumeandaa semina hii ili kuwakutanisha wafanyabiashara wadogo na wa kati na wato huduma za kifedha nchini kubadilishana uzoefu na kujadili ugumu wa upatikanaji wa mikopo na kuona namna ambayo tunaweza kurekebisha hali hiyo kupitia maboresho ya sera, sheria na kanuni husika za nchi."Alisema Akaro

"Hawa ndio watengezaji ajira lakini ukuaji wake umekuwa ni mdogo na hivyo kuathiri ukuaji wa uchumi na fursa za ajira, tunakaa na wadau tuweze kujua ugumu uko wapi na kutenegenza maazimio yatakayowasilishwa seriklai kwa ajili ya hatua stahiku."Aliongeza

Ameyataja malengo mahsusi ya semina hiyo kuwa ni pamoja na kupanua uelewa  wa vyanzo vya mikopo na jinsi kupata huduma zinazolenga biashara ndogo na kati, kushawishi wadau kuboresha upatikanaji wa mitaji na huduma nyengine za kifedha kwa biashara na kushawishi serikali kuharakisha uboreshaji usimamizi wa sekta ya fedha.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa Vodacom Rosalynn  Mworia amesema shabaha ya semina hiyo inaendana na ajenda ya Vodacom ya uwepo wa urahisi wa upatikanajai wa huduma za fedha nchini kw anamna iliyo rahisi na yenye uwezo wa kufikiwa na kila mmoja wakiwemo wafanyabiashara wadogo na kati ili kurahisisha ustawishaji uchumi na maisha ya watu kupitia huduma ya M-pesa.

Mworia amesema M-pesa imeonesha mageuzi makubwa katika uendeshaji wa biashara hapa nchini kwa kuwa kiungo muhimu kati ya wafanyabiashara na watoa huduma za fedha kwa upande mmoja na kati ya wafanyabiashara hao na wateja na soko kwa upande wa pili.

"M-pesa inabeba ajenda ya urahishaji upatikanaji wa huduma za fedha hapa nchini. Leo tunapozungumzavipo vithibitisho vya wazi jinsi huduma hiyo ilivyoleta mapinduzi makubwa hapa nchini nasi kwetu hali inatutia moyo na kuongeza juhudi za uetekelzaji wa ajenda hii kwa masilahi ya nchi."Alisema Mworia

Amesema kupitia M-pesa wafanyabiashara wamekuwa na urahisi wa kufanya miamala yao huku wakiunganishwa kwa namna ya kipekee na mabenki na taaisis nyengine za kifedha kazi ambayo Vodacom itaendelea kuifanya ikiwemo kwa kushirikiana na wadau wengine.

Nae Mtaalamu wa Biashara ndogo na za kati wa FSDT Peter Kingu amesifu wazo la kubuniwa kwa semina hiyo na kwamba taasisi yake itaendelea kuunga mkono ubunifu wa aina hiyo.