Sunday, December 14, 2014

WWF YAMWAGA VIFAA VYA BUSTANI KWA SHULE ZA MUFINDI


WWF YAMWAGA VIFAA VYA BUSTANI KWA SHULE ZA MUFINDI
 Wanafunzi wa shule ya msingi Igomaa wilaya ya Mufindi wakipata maelekezo ya namna ya kuanzisha vitalu cha bustani ya miti kutoka mtaalam.

Ofisa Maendeleo ya jamii msaidizi Bi. Martha Sanga akigawa vifaa ya bustani kwa mwalimu wa shule ya sekondari sadani.

Ofisa Maendeleo ya jamii msaidizi Bi. Martha Sanga akiongea na wanafunzi

Na Friday Simbaya, Mufindi

Shirika la Hifadhi ya Mazingira Duniani (WWF) kupitia Programu ya Maji Ruaha (RWP), mkoani Iringa limekabidhi vifaa kwa ajili ya kuanzisha vitalu vya bustani za miti katika shule mbalimbali za Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa.
Ofisa Maendeleo ya Jamii msaidizi wa shirika hilo, Martha Sanga alisema vifaa vilivyotolewa ni pamoja na tolori,water can,leki, viliba, majembe, chepe na mbegu aina saba za miti, ambavyo vilikabidhiwa kwa kamati za mazingira za shule.
Shule zilizopewa nyenzo hizo ni pamoja na Shule ya Sekondari Sadani, Shule ya Msingi ya Igomaa na Shule ya Sekondari Isalavanu.
Alisema kuwa zaidi ya shilingi milioni tatu (3m/-) zilitumika kwa ajili ya vifaa pamoja na malipo ya wawezeshaji, mafuta ya gari na mengineyo.
Alisema kuwa wameamua kutoa vifaa hivyo kwa shule ilikupandiza mbegu ya uhifadhi kwa watoto wa shule na hatimaye kupeleka elimu ya kutunza mazingira kwenye familia zao. na imeshindwa kutunza miti ya matunda katika mashamba darasa hayo zilizotolewa na shirika hilo.
"Tuliwahi kuipa jamii mbegu za miti ya matunda iliweze kuanzisha bustani za matunda wakashindwa kuitunza na kwa safari hii tumeamua kuwapa wanafunzi vifaa vya bustani kupitia kamati zao za mazingira kwa sababu ni rahisi kutunza mazingira," alisema Sanga.
Naye mtaalamu kutoka idara ya ardhi na maliasili kitengo cha misitu, Khalid Kayowa wa halmashauri ya wilaya Mufindi alitoa mafunzo kwa kamati za mazingira hizo ya namna ya kutumia vifaa pamoja na namna ya kutungeza vitalu vya miche.
Alivitaja vitu vinavyohitajika kuanzisha eneo la kuwatika mbegu za miti kuwa ni udongo,mchanga, mbolea ya mbonji pamoja na viliba na madawa kwa ajili ya kuulia wadudu na lazima na kivuli cha kutosha pamoja kuwe na uzio.
Alisema kuwa kamati za mazingira hizo hazinabudi ya kufuata ushauri wa kitaalamu ya namna ya kuanzisha bustani kwa ajili ya kuzalishia miche ya miti itakayopandwa katika maeneo mbalimbali shule.
Shirika la WWF limejikita katika kuhamasisha shughuli za utunzaji wa mazingira, rasilimali za maji, pamoja na maendeleo ya jamii, ikiwemo kilimo, ambapo limekuwa likishiriki kikamilifu katika utoaji wa elimu na vifaa kwa wanajamii.

"Mto Ruaha Mkuu ndiyo chanzo kikuu cha maji katika bwawa la Mtera ambako kuna mitambo ya kuzalisha umeme na lengo kubwa ni kuhakikisha mto huo unatililisha maji kwa mwaka mzima" alisema ofisa maendeleo ya jamii msaidizi.

WWF huendesha Programu ya Maji (RWP) katika wilaya nane ambazo ni Iringa Vijijini, Kilolo, Mufindi, Njombe, Mbarali, Mbeya Vijijini, Chunya na Makete.

Hivi karibuni Shirika la Hifadhi ya Mazingira Duniani (WWF) kupitia Programu ya Maji Ruaha (RWP), mkoani Iringa lilikabidhi vifaa vya upaliliaji wa zao la mpunga kwa wakulima wa Kata ya Mlenge, Tarafa ya Pawaga wilayani Iringa.

Vifaa vilivyotolewa vitakavyosaidia kupalilia pamoja na kuwanufaisha wakulima wa mpunga wa Skimu ya Umwagiliaji ya Mlenge, kutoka vijiji vya Kinyika, Isele, Kisanga na Magombwe.