"Mhisani anayekusaidia kujijengea uwezo wa kujitegemea ni muhimu sana kuliko Yule anayekupatia msaada kila siku bila kukujengea uwezo wa kusimama mwenyewe na kujitegemea"anasema Bw.Omar Abdul Kyaruzi Katibu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Mwandaliwa kilichopo eneo la Boko wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam kutokana na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania kusaidia kituo hicho kujenga banda la kisasa kwa ajili ya kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku.
Mbali na kufadhili ujenzi wa banda la kuku pia wafanyakazi wa Vodacom Tanzania katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja inayoendelea wamejitolea muda wao kushiriki katika ujenzi wa banda hilo la kisasa ambalo lina ukubwa wa kufugiwa kuku wapatao 2,000 kwa pamoja.
Afisa Mwandamizi wa Vodacom Tanzania kutoka kitengo cha Huduma kwa wateja Benson Megehema, amesema kuwa wiki hii mbalimbali na kuongea na wateja na kuwaelimisha huduma bora zinazotolewa na kampuni pia wameona ni muhimu kutenga muda wao kusaidia shughuli za kijamii hususani kusaidia wahitaji kwenye jamii.
"Kwetu Vodacom kusaidia jamii ni moja ya sera yetu na siku zote tutakuwa mstari wa mbele kusaidia jamii tunayoishi na kufanyia biashara na tunaamini kuwa kusaidia sio kutoa fedha tu bali ni kujitoa muda wetu pia kujumwika na watoto hawa wapatao themanini na kitu na kuweza kusaidia shughuli za kijamii kwani tunatambua uhitaji wetu ni muhimu sana kwa watoto hawa tukiwa na lengo la mradi huu kuweza kuwasaidia katika mahitaji yao ya hapa na pale"Anasema Magehema.
Kwa upande wake Katibu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Mwandaliwa,Bw.Omar Kyaruzi,alisema kuwa wanashukuru kampuni ya Vodacom Tanzania kwa kuona umuhimu wa kuweajengea banda kwa ajili ya uanzishaji wa mradi wa ufugaji wa kuku.
Pia aliongeza kuwa wamefarijika kuona wafanyakazi wa Vodacom wanaacha kazi zao ofisini na kuungana na mafundi katika kazi ya ujenzi "Suala hili limetutia moyo sana hata watoto tunaowalea wamejifunza kuwa msaada sio kutoa fedha peke yake bali kutumia muda wako kusaidia jamii ni msaada mkubwa kwa kuwa wakati ni pesa"Alisema Kyaruzi.
Kyaruzi alisema kuwa Kituo cha watoto yatima cha Mwandaliwa kinatoa malezi kwa watoto yatima na kimekuwa kikitegemea kujendesha kupitia misaada mbalimbali inayotolewa na wafadhili.
Katibu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Mwandaliwa cha Bunju jijini Dar es Salaam, Bw.Omar Abdul Kyaruzi(kushoto)akimpa maezo Meneja wa Vodacom Foundation,Grace Lyon jinsi ujenzi wa banda la kisasa kwa ajili ya kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku unaufadhiliwa na taasisi ya Vodacom foundation unavyoendelea kituoni hapo walipotembelewa na wafanyakazi wa Vodacom katika kushiriki kwenye ujenzi huo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja duniani.
Wafanyakazi wa Idara ya huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania,wakishiriki katika ujenzi wa banda la kisasa kwa ajili ya kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku kwenye kituo cha kulelea watoto yatima cha Mwandaliwa kilichopo Bunju, jijini Dar es salaam,Wafanyakazi hao walishiriki katika ujenzi huo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja duniani.