Thursday, October 09, 2014

NHIF yapima afya bure wananchi wiki ya vijana Tabora


NHIF yapima afya bure wananchi wiki ya vijana Tabora
Mkuu wa Mkoa wa Tabota Fatuma Mwasa akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya katika maonesho ya wiki ya vijana yanayofanyika kitaifa mkoani humo, aliyesimama ni Meneja wa Mfuko Mkoa wa Tabora.
Vijana wakiwa kwenye banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wakipima afya zao. Katika maonesho hayo Mfuko unaendesha zoezi la upimaji afya bure.
Mtaalam wa macho Antony Janken akimpima macho Rehema Majaliwa ambapo huduma ya macho pia inatolewa bandani hapo. 
Kijana John Masanja akipata vipimo na ushauri wa kuepukana na maradhi yasiyoambukiza bandani hapo.