Monday, October 27, 2014

Kumbukumbu ya Commando Luteni Rajab Ahmed Mlima



Kumbukumbu ya Commando Luteni Rajab Ahmed Mlima
 Leo katika kukumbuka siku ya Commando Luteni Rajab Ahmed Mlima, katika kumuenzi  wanafamilia wanafanya usajili wa "  Luteni RAJAB Ahmed MLIMA FOUNDATION."

Commando Luteni Rajab Mlima akiwa katika Special Forces ya Tanzania ndani ya Jeshi la kulinda Amani la Umoja wa Mataifa alifariki dunia katika mapambano na waasi wa M23 siku chake kabla ya kutomezwa kwa kundi hilo huko Kiwanja nchini DRC.

Luteni Rajab Mlima Foundation, itasimamia na kuendeleza mambo muhimu kwa jamii ambayo Luteni Rajab Mlima katika uhai wake aliyapa kipaumbele kama masuala ya elimu nakadhalika.

Zifuatazo nimbaadhi ya picha za Luteni Rajab Mlima katika uhai wake na akiwa katika mafunzo na kazi za kulinda amani.

Mwenyezi Mungu amweke mahali pema peponi.
Imetolewa na familia.