Kivuko cha Msangamkuu(                MV Mafanikio) chenye uwezo wa kubeba uzito wa tani 50                pamoja na abiria 100 kikiwasili Mkoani Mtwara tayari kwa                kuanza kazi rasmi ya kutoa huduma kati ya upande wa Mtwara                Mjini na Msangamkuu. 
                Kivuko kipya cha (MV                Mafanikio) kama kinavyoonekana mara baada ya Serikali                kutekeleza ahadi yake ya kuwaletea wananchi wa Mtwara                Kivuko hicho kipya. 
                Wananchi wakikimbia                kuingia ndani ya Kivuko hicho kipya cha (MV Mafanikio)                huku wakishangilia kuonyesha furaha yao mara baada ya                kivuko hicho kuwasili mkoani Mtwara. 
                Baadhi ya kina mama nao                walipata fursa ya kukaa na kufurahia ndani ya kivuko hicho                kipya. 
                Usafiri huu wa Mitumbwi                ndio uliokuwa unategemewa na wananchi hao wa Mtwara kabla                ya ujio wa Kivuko kipya cha Msangamkuu. 
                Mkurugenzi wa Ufundi na                Umeme (DTES) Dkt. Wiliam Nshama kutoka Wizara ya Ujenzi                akipita kukagua Kivuko hicho kipya cha Mv Mafanikio. Picha                zote kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano                Serikalini-Wizara ya Ujenzi.