Cardinal Rugambwa Social Centre ni ukumbi mpya wa sherehe ambao umeanza kazi pale pembeni pa Kanisa la Mtakatifu Peter (St. Peter's) jijini Dar es salaam, ambao unaongeza idadi ya kumbi za aina hiyo zenye kila kitu cha kisasa. Na tayari umekuwa kimbilio la wadau wengi wenye sherehe mbalimbali.
Usiku wa kuamkia leo Ankal alikuwepo kwenye ukumbi hio maridadi katika mnuso wa send off uliohudhuriwa na wadau kibao, akiwemo Baba Paroko wa kanisa hilo Fr. Kaombwe (kushoto kwa Ankal) ambaye pamoja na hao wadau wengine ni wadau wakubwa wa Globu ya Jamii. |
Ankal na wadau wakiwa kwenye ukumbi huo maridadi wa Cardinali Rugambwa katika mnuso wa send off uliohudhuriwa na wadau kibao.