Mwenyekiti UVCCM mkoa wa Arusha Robinson Meitinyiku akitoa taarifa ya ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya taarifa za upotoshaji zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari na baadhi ya viongozi wa UVCCM mkoani hapa. Ambao Mkutano huo ulitanguliwa na Kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Arusha waliaofikiana kutoa maamuzi juu ya mgogoro wao na Kaimu Katibu wa UVCCM Mkoa wa Arusha Gerald Mwadalu anayetuhumiwa kufunga ofisi na matumizi mabaya ya fedha za umoja huo.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Karatu Ally Rajabu akisoma maazimio ya Kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Arusha lililokutana leo na kutoa maazimio 17 likiwamo la kumpiga marufuku Kaimu Katibu UVCCM Mkoa wa Arusha Gerald Mwadalu asijihusishe na kazi za UVCCM mkoa wa Arusha.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa UVCCM Mkoa wa Arusha Diwani Kimayi (katikati) pamoja na wajumbe wenzake wakisikiliza maazimio yaliyokuwa yakisomwa ambapo kwa upande wake alitoa ushauri kwa Baraza Kuu la Taifa la UVCCM kwamba linapoteua watendaji lie linaangalia watendaji wenye sifa.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatulia maazimio yaliyofikiwa na Kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Arusha kilichofanyika leo jioni.Ambapo Baraza hilo liliazimia kuanza kufanyiak kwa ukaguzi wa mara kwa mara katika ofisi za UVCCM mkoa kwa kila mwezi kwa ajili ya kdhibiti ubadhilifu.
Baadhi ya wajumbe wa Kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Arusha wakifuatilia maazimio yaliyokuwa yakisomwa mbele ya wanahabari leo mjini hapa ambapo Baraza hili liliazimia kwamba endao Katibu wa Mkoa Mary Chatanda atabainika kuwa na ubadhilifu basi asihamishwe mkoa mwingine na apelekwe mahakamani ili iwe fundisho.
picha kwa hisani ya woindeshizza blog