Thursday, July 03, 2014

BENKI YA CRDB TAWI LA BABATI LAANZA KUTOA HUDUMA ZA KIBENKI




BENKI YA CRDB TAWI LA BABATI LAANZA KUTOA HUDUMA ZA KIBENKI
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Elaston Mbwilo akiwa na wadau mbalimbali wa mkoa huo, wakiwa kwenye Tawi la Babati la Benki ya CRDB ambalo jana lilianza kutoa huduma ya fedha kwa wateja wake, kulia kwake ni Meneja wa CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa na kushoto ni Katibu Tawala wa mkoa huo Omary Chambo na kushoto kwa RC Mbwilo ni DC wa Babati Khalid Juma Mandia na Katibu wa CCM wa Mkoa huo Ndeng'aso Ndekubali.  (PICHA
NA WOINDE SHIZZA,MANYARA.
Baadhi ya wadau walioshiriki ufunguzi wa huduma za fedha kwenye Benki
ya CRDB Tawi la Babati Mkoani Manyara, ambalo jana lilianza kutoa
huduma za fedha kwa wateja ikiemo kuweka akiba, kutoa fedha na
kuchukua mikopo, ambapo linatarajiwa kufanyiwa uzinduzi wake hivi
karibuni.
 Meneja wa Benki CRDB Tawi la Babati Mkoani Manyara, Ronald Paul
akizungumza na waandishi wa habari ambapo kwa mara ya kwanza Tawi hilo lilianza kutoa huduma ya fedha kwa wateja wake jana na linatarajia
kuzinduliwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda au Rais Jakaya Kikwete.
Baadhi ya Maofisa wa Jeshi la JWTZ wakipata maelezo mbalimbali kuhusiana na huduma za kibenki ndani ya Benki ya CRDB Tawi la Babati Mkoani Manyara, lilipoanza kutoa huduma ya fedha kwa wateja mbalimbali mkoani humo ikiwemo kuweka akiba, kutoa fedha na kutoa mikopo.

 ===========  ========  =======

Na Woinde Shizza,Manyara.

Wananchi wa Mkoa wa Manyara, wametakiwa kutumia fursa ya kuwepo kwa huduma ya benki ya CRDB Tawi la Babati, kwa kujiwekea akiba na kuchukua mikopo kwa lengo la kujinufaisha kiuchumi na kuongeza pato la Taifa.

Mkuu wa mkoa wa Manyara, Elaston Mbwilo aliyasema hayo wakati wa zoezi la benki ya CRDB tawi la Babati, lilipoanza kutoa huduma ya fedha kwa wateja wake na yeye kuwa mtu wa kwanza kuweka fedha kwenye tawi hilo.

Mbwilo aliwataka wananchi wa mkoa huo kufungua akaunti za fedha kwenye benki tofauti ikiwemo CRDB, NMB, NBC, Posta na Exim, ambazo zipo mjini Babati, kuliko kuweka kwenye benki moja na kuitegemea yenyewe pekee.

"Waswahili wanasema usiweke mayai yote kwenye kapu moja, hivyo tutumie fursa hii kwa kuweka akiba katika benki tofauti tofauti, hapa unaweka sh200, kule sh300, pengine sh100 ndiyo nidhamu ya fedha ilivyo," alisema Mbwilo. Hata hivyo, alisema Waziri Mkuu Mizengo Pinda au Rais Jakaya Kikwete mmoja wao ndiye atakayekuja kulizindua rasmi Tawi hilo na alitoa wito kwa benki hiyo ya CRDB kuanzisha matawi mengine kwenye wilaya za mkoa wa Manyara.

"Siku za nyuma tulikuwa tunaona gari la benki linakuwa hapa kwa wiki mara moja ila sasa mmeweza kuweka Tawi hapa Babati, sambaeni na sehemu nyingine huko wilayani msogeze huduma hizi karibu na jamii," alisema Mbwilo. Naye, Meneja wa CRDB Tawi la Babati Ronald
Paul aliwataka wafanyabiashara, watumishi, wakulima na wafugaji wa
mkoa huo kutumia fursa ya kuwepo kwa benki hiyo kwa ajili ya kupata huduma za kifedha ikiwemo kuweka akiba.

"Jamii itumie nafasi hii kwa kuweka na kutoa fedha na pia hapa Babati ni kwenye barabara kuu hata viongozi wengi wanapita kuelekea Dodoma, hivyo watatumia fursa hii ya kuwepo kwa tawi letu kupata huduma ya fedha," alisema Paul.