Thursday, July 03, 2014

WIZARA YA NISHATI NA MADINI YANG’ARA KWENYE MAONESHO YA SABA SABA



WIZARA YA NISHATI NA MADINI YANG'ARA KWENYE MAONESHO YA SABA SABA
Mjiolojia Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. Mwara Shoo akitoa maelezo kwa mmoja wa wananchi waliotembelea banda la Wizara ya Nishati na Madini kwenye maonesho ya kimataifa ya Saba Saba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Afisa Utaalam Elekezi kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Advera Mwijage akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda hilo.
Wataalam kutoka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mstaafu wa Shirika hilo Bw. Gray Mwakalukwa mara alipotembelea banda hilo.
Mjiolojia Mkuu kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) Bw. Momburi Philip akitoa elimu kwa mwananchi aliyetembelea banda hilo.
Mtaalam kutoka Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Mhandisi Juliana Palangyo akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mstaafu wa Shirika la Madini la Taifa Bw. Gray Mwakalukwa mara alipotembelea banda hilo.
Mtaalam wa Mazingira kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA) Bi. Monica Augustino akitoa maelezo kwa kikundi cha kinamama wajasiriliamali kutoka Simanjiro mara walipotembelea banda hilo.
Mjiofizikia kutoka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Bw. Denis Silas akitoa ufafanuzi juu ya shughuli za shirika hilo kwa mmoja wa wananchi waliotembelea banda hilo.
Mtaalam kutoka Kitengo cha Uthamini wa Madini ya Almasi na Vito (TANSORT) Bi. Teddy Goliama (kulia) akitoa elimu kwa mwananchi aliyeshika kinyago jinsi shughuli za uthamini wa madini ya vito zinavyofanywa na Kitengo hicho.
Mtaalam kutoka Kitengo cha Uthamini wa Madini ya Almasi na Vito (TANSORT) Matiko Mwita Sanawa akimwonesha kinyago kilichotengenezwa na madini mmoja wa wananchi waliotembelea banda la Wizara kwenye maonesho hayo.