Thursday, July 03, 2014

VODACOM NA CRDB BENKI WAZINDUA HUDUMA MPYA YA M-PESA


VODACOM NA CRDB BENKI WAZINDUA HUDUMA MPYA YA M-PESA
Mkurugenzi wa Huduma Mbadala za Benki wa CRDB Joseph Witts akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya kutoa pesa kwenye M-pesa kupitia ATM za benki bila kuhitaji kuwa na kadi wala akaunti ya beki hiyo. Wengine pichani ni Ofisa Mkuu wa Biashara Mtandao wa Vodacom Jacques Voogt na Meneje Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim.
Ofisa Mkuu wa wa Biashara Mtandao wa Vodacom Jacque Voogt akittumia ATM ya Benki ya CRDB kutoa pesa kwenye akaunti ya M-pesa katika simu yake ya mkononi muda mfupi baada ya kuzinduliwa kwa huduma hiyo mpya. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma Mbadala za Benki wa CRDB Joseph Witts. Huduma hiyo humuwezesah mteja yoyote wa M- pesa kutumia ATM za benki hiyo kuchukua pesa bila kujali kama ni mteja wa CRDB.
Mkurugenzi wa Huduma Mbadala za Benki wa CRDB Joseph Witts akitumia ATM ya Benki ya CRDB kutoa pesa kwenye akaunti ya M-pesa katika simu yake ya mkononi muda mfupi baada ya kuzinduliwa kwa huduma hiyo mpya. Kushoto ni Ofisa Mkuu wa Biashara Mtandao wa Vodacom Jacques Voogt. Huduma hiyo humuwezesha mteja yoyote wa M-pesa kutumia ATM za CRDB popote nchini kutoa pesa hata kama si mteja wa benki hiyo.
Ofisa Mkuu wa wa Biashara Mtandao wa Vodacom Jacques Voogt na Mkurugenzi wa Huduma Mbadala za Benki wa CRDB Joseph Witts (katikati wenye suti nyeusi) wakipongezana baada ya kuzindua huduma m-pya ya kutoa pesa kwenye M-pesa kupitia ATM za CRDB nchi nzima. Wengine pichani ni wafanyakazi wa Vodacom na wa Benki ya CRDB. Huduma hiyo huweza kutumiwa na mteja yeyote wa M-pesa hata kama si mteja wa benki hiyo.