Mteja akipata maelezo ya Kina kutoka kwa wafanyakazi wa Access Bank katika banda lao lililopo kwenye maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni ya Channel 10, Meshack akifanya mahojiano na Ofisa Masoko Mwandamizi wa Access Bank, Muganyizi Bisheko na kueleza huduma wanazozitoa katika banda lao lililopo kwenye maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Ambapo Bisheko alisema kuwa huduma zinazotolewa ndani ya banda lao ni ufunguaji wa akaunti kwa bei rahisi ya shilingi 1,000 huduma ya utoaji wa mikopo kwa wajasiliamali Mtangazaji wa Azam Tv, Wasiwasi Mwabulambo akizungumza machache ndani ya banda la Access Bank mara baada ya kutembelea katika banda lao lililopo kwenye maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Wa pili kutoka kulia ni Afisa Masoko Mwandamizi wa benki hiyo, Muganyizi Bisheko akiwa pamoja na wafayakazi wenzake.
Wafanyakazi wa Acces Benki wakipata pozi mbele ya kamera ya Kajunason