Wananchi wapatao 350 waliokuwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kijiji cha Msange, Jimbo la Singida Kaskazini, Wilaya ya Singida Vijijini, mkoani Singida wakiwa wameshika kadi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) huku wakila kiapo cha uzalendo baada ya kujiunga na chama hicho kwenye moja ya mikutano ya 'Operesheni Delete CCM' uliohutubiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zanzibar, Salum Mwalimu, mwishoni mwa wiki. Sehemu ya Umati Mkubwa Ukimsikiliza Mwenyekiti Taifa wa Taifa wa Chadema Freeman Mbowe alipohutubia mikutano mitano kwenye majimbo matatu ya Ulanga Magharibi, Ulanga Mashariki na Kilombero.Mikutano yote ilikuwa mikubwa sana na yenye hamasa kubwa huku wenyeviti saba wa CCM wa vijiji kwenye jimbo la Ulanga Mashariki wakirudisha kadi za CCM na kujiunga na CHADEMA na kuahidi kuongeza nguvu zaidi kwenye Operation Delete CCM ambapo watasaidia wagombea watakao simamishwa na Chadema pamoja na vyama vingine vya UKAWA.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akiwahutubia wanachi wa kijiji cha Nyandila kilichopo juu ya milima ya Uruguru mkoani Morogoro, katika mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM juzi. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akiwahutubia maelfu ya wananchi wa mji wa Mtibwa katika jimbo la Mvomero mkoani Morogoro, katika mkutano wa hadhara wa Operesheni Delete CCM juzi Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akilakiwa na wanachi wa mji wa Gairo mkoani Morgoro baada ya kuwasili, ambako alifanya mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM juzi. 
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zanzibar, Salum Mwalimu akiwalisha kiapo cha uzalendo wanachama wapya katika Kijiji cha Msange, Jimbo la Singida Kaskazini, Wilaya ya Singida Vijijini, mkoani Singida waliohama kutoka Chama Cha Mapinduzi, katika moja ya mikutano 'Operesheni Delete CCM', uliofanyika mwishoni mwa wiki kijijini hapo,Picha na Chadema