Thursday, May 22, 2014

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA MAJI, YAZINDUA MWONGOZO WA UTENDAJI KWA MAMLAKA ZA MAJI NCHINI

 
Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Injinia Mbogo Mfutakamba (katikati) wakati wa akizindua chapisho la Kanuni na utaratibu wa kuzingatia kwa Mamlaka zinazohusika na usimamizi na usambazaji wa maji nchini wakati wa mkutano wa mwaka wa wataalaam na watendaji wa usimamizi wa sekta ya maji nchini.
Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Injinia Mbogo Mfutakamba (katikati) akiwaonesha wataalam na watendaji wa usimamizi wa sekta ya maji nchini chapisho la Kanuni na utaratibu wa kuzingatia kwa Mamlaka zinazohusika na usimamizi na usambazaji wa maji nchini wakati wa mkutano wao wa mwaka jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Uwezeshaji wa Maendeleo ya Miradi ya Maji kutoka shirika la GIZ nchini Dkt. Fred Lerise akitoa ufafanuzi kwa wataalam wa maji kuhusu chapisho la Kanuni na utaratibu wa kuzingatia kwa Mamlaka zinazohusika na usimamizi na usambazaji wa maji nchini wakati wa mkutano huo wa mafunzo wa mwaka uliowahusisha wataalam na watendaji wa mamlaka za maji kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Mtendaji wa Shirikisho la Wasambazaji wa Maji nchini (ATAWAS) Bi. Martha Kabuzya akizungumzia umuhimu wa chapisho hilo kwa sekta ya maji nchini na kutoa wito kwa mamlaka zote nchini kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuhakikisha kuwa wateja wanaowahudumia wanapata huduma bora.
Sehemu ya Wataalam nawatendaji wa Mamlaka zinazohusika na usimamizi na usambazaji wa maji nchini waliohudhuria mkutano wa mwaka wa wataalaam na watendaji wa usimamizi wa sekta ya maji nchini. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.