Tuesday, September 11, 2012

NAIBU WAZIRI UJENZI AKAGUA MAENDELEO YA MIRADI YA UJENZI WA BARABARA LEO JIJINI DAR



 
Naibu waziri wa Ujenzi Gerson Lwenge (kushoto) akitoa maelekezo kwa mkandarasi anayejenga barabara inayopita eneo la Jangwani,Kigogo na kuelekea kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha ubungo yenye urefu wa km 6.4 Injinia Abdul Kimaro (kulia kwa naibu waziri) leo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya barabara jijini Dar es salaam.
 
Mhandisi wa Miradi kutoka wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Ntije Nkolante (kulia) akimwonyesha Naibu Waziri wa Ujenzi Gerson Lwenge (aliyenyosha mkono kushoto) sehemu ya mwinuko ambayo iko kwenye matengenezo katika barabara iendayo Yombo Vituka yenye urefu wa kilometa 10.3 inayojengwa na kampuni ya Nyanza Roads Work leo jijini Dar es salaam.
 
Mkandarasi anayejenga barabara ya Jangwani,Kigogo kuelekea kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha ubungo Mhandisi Abdul Kimaro (katikati) akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Ujenzi Gerson Lwenge juu ya maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo na changamoto zinazokwamisha kukamilika kwa muda uliopangwa.
 
Sehemu ya barabara ya Yombo Vituka ambayo ujenzi wake umekamilika yenye urefu wa kilometa 10.3 inayojengwa na kampuni ya Nyanza Roads Work jijini Dar es salaam.
 
Eneo la Davis Corner, Vituka jijini Dar es salaam ambalo baadhi ya wakazi wanalitumia kutupia taka kinyume cha sheria. Eneo hili litajengwa mzunguko (Round about) na kuyawezesha magari kupita katika eneo hilo na kupunguza msongamano wa magari katika eneo hilo katika mikakati inayoendelea ya kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es salaam.Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.