Thursday, March 17, 2016

NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI AWATAKA JESHI LA POLISI MWANZA KUTENDA UADILIFU NA KUFUATA MAADILI YA KAZI



NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI AWATAKA JESHI LA POLISI MWANZA KUTENDA UADILIFU NA KUFUATA MAADILI YA KAZI
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na viongozi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza mara baada ya kuwasili jijini hapo jana akitokea mkoani  Kagera kwa ziara ya kikazi.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni akisaini katika kitabu mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Mwanza,mara baada ya kuwasili jijini hapo  jana akitokea Kagera kwa ziara ya kikazi.
 Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza,ACP Japhet Lusingu(kushoto), akitoa taarifa ya hali ya usalama katika mkoa wa Mwanza kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(katikati) mara baada ya Naibu Waziri kuwasili jijini Mwanza jana akitokea mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi.Kulia ni Mkuu wa Upelelezi na Makosa ya Jinai mkoa wa Mwanza,SSP Augustine Senga.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na baadhi ya viongozi wa Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza mara baada ya kuwasili jijini hapo jana akitokea Kagera kwa ziara ya kikazi.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi) .Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi