Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama (kushoto) akimkabidhi msaada wa fedha taslimu sh. milioni moja mchezaji wa zamani wa Simba, Mtibwa na Taifa Stars, Alphonce Modest kwa ajili ya kumsaidia katika matibabu ya ugonjwa wa mifupa unaosababisha miguu kufa ganzi ‘yabisi baridi’. Modest nasumbuliwa na ugonjwa huo tangu mwaka 2011. Kwa yeyote anayeguswa na tatizo lake awasiliane na mtangazaji wa Chanel 10, Said Kilumanga (wa pili kulia) kwa kupitia namba 0718 427426. Wa Pili kushoto ni Mhariri Kiongozi wa Champion, Saleh Ally.
Mtangazaji wa Channel 10, Said Kilumanga akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa rai kwa watu mbalimbali kujitolkeza katika kumsaidia mchezaji wa zamani wa Simba na timu ya Taifa Alfonce Modest ambaye anasumbuliwa na matatizo ya miguu.
Beki wa zamani wa Simba na timu ya Taifa, Alfonce Modest akimshukuru Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions baada ya kumsaidia kiasi cha sh milioni moja kwa ajili ya kuanza matibabu ya miguu.